Meneja
wa Nyanda za juu kusini wa airtel tanzania Bw, Beda Kinunda akipokea
cheti cha heshima toka kwa Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Dr
Emainuel John Nchimbi wakati wa ufunguzi rasmi wa Maadhimisho ya wiki ya
usalama barabarani mkoani Iringa kwaajili ya kuhamasisha jamii
kuzingatia sheria barabarani katika viwanja vya Samora mkoani hapo.
Maadhimisho
ya wiki ya usalama barabarani yamefanyika Rasmi mkoani Iringa huku
maandamano maalum kwaajili ya kuhamasisha jamii kuzingatia sheria
barabarani yakifanyika katika viwanja vya Samora mkoani hapo.
Katika
maadhimisho hayo kampuni ya simu za mkononi ya Airtel ilikabidhiwa cheti
cha kushiriki na kuwa wadau wazuri wa usalama Barabarani
Akiongea
katika maadhimisho hayo Katibu Mwenezi wa Usalama barabarani Bw, Heri
Bantu ameyataka makampuni na taasisi mbalimbali kuiga mfano wa kampuni
ya Airtel kwa kutoa mchango wa hali na mali katika kupunguza ajali
Barabarani . aidha amewataka wananchi wote kuwa makini kwa kuzingatia
Sheria na Kanuni za Usalama Barabarani,
Mara
baada ya kukabidhiwa cheti cha Heshima kwa mchango Airtel Tanzania
wamesema wataendelea na kampeni yao ya kuhakikisha ujumbe wa usalama
barabarani “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
unafikia walengwa wote kupitia njia mbalimbali za mawasiliano
“Airtel
Tanzania tunaendelea na dhamira yetu ya kuhakikisha Usalama barabarani
pamoja na kupunguza vifo vya ndugu zetu kutokana na ajali
vinapungua,hivyo tumeanza kutuma ujumbe mfupi (SMS) kwa wateja wetu
nchini kuwasihi kuheshimu sheria barabarani ili kuokoa maisha ya wengine
alisema Mmbando Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania
Airtel
Tanzania ni wadhamini wa kampeni hii ya nenda kwa usalama barabarani kwa
miaka mitano mfululizo sasa na kwa mwaka huu Airtel imejitolea
uchapishaji wa stika za usalama barabarani pamoja hilo pia Airtel
imeshaweka mabango yenye kutoa tahadhari za barabara kwa abiria na
madereva katika barabara mbalimbali zilizopo nchini kwa lengo la
Kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment