Mohammad Ali.
Bingwa wa Dunia wa zamani wa mchezo wa ngumi wa Marekani Muhammad Ali, ametunukiwa medali ya uhuru mjini Philadelphia.
Muhammad Ali amekabidhiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika katika kituo cha taifa cha katiba.
Tuzo
hiyo inatambua mchango wa muda mrefu wa Muhammad Ali kama mpiganaji nje
ya viwanja vya kupigana ndondi kwa ajili ya binaadamu, haki za kiraia
na uhuru wa dini.
Bondia
huyo ambaye kwa sasa afya yake imedhoofika, hakuongea, lakini
alisaidiwa kusimama na kupokea medali hiyo kutoka kwa binti yake Laila.
Mkewe Lonnie alisema Ali amefarijika kwa kutambuliwa kama mnara wa taa ya uhuru.
Tangu
kustaafu kupigana ngumi mwaka 1981, Ali ametembelea sehemu mbalimbali
duniani kwa kazi za misaada ya kiutu na ametumia muda wake mwingi katika
kazi za kijamii.
Aidha
watu wengine waliyowahi kupata tuzo hiyo ni pamoja na rais rais mstaafu
wa Afrika Kusini Nelson Mandela na Jimmy Carter wa Marekani.
No comments:
Post a Comment