Mmoja
wa viongoi wa maandamano hayo jina lake halijaweza kupatikana kwa
haraka akiwahimiza waislam wenzake kuto kukata tamaa moaka kieleweke.
Hapa wakiwa mbele ya jengo la wizara ya Mambo ya ndani kama
linavyoonekana kwa mbele
Wakina
mama wa kiislam nao hawakuwa nyuma katika maandamano hayo wakishinikiza
waislam wenzao waliokamatwa kwa sababu ya kugoma kuhesabiwa watolewe,
mpaka hivi sasa tunaingia mitamboni bado waandamanaji hao wapo katika
jengo hilo la Wizara ya mambo ya ndani.
Wanahabari nao hawakua nyuma katika kupata picha za tukio hilo
Kwa
juu kwenye gorofa ni wafanyakazi wa Benk ya Exim iliyo karibu na Wizara
hiyo wakiwa hawajui la kufanya huku wengi wao wakihofu kama mabomu ya
machozi yakianza kupigwa watajisalimisha wapi, huku waislam kama
unavyowaona kwa chini wakiwa wanaimba nyimbo mbali mbali za
kuhamasishana kama iivyozoeleka kwa usemi wa kiimani yao
"TAKHBIIRRR!!!!"
Hapa wakiwa wanaelekea kwenye wizara ya mambo ya Ndani.
Tikio
hilo limetokea muda mfupi uliopita. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote
ambayo imetolewa na jeshi la polisi kutokana na maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment