Msanii wa muziki wa kizazi kipya Cirryl a.k.a Kamikazi akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012.
Ni Kushangweka tu ndani ya viwanja vya Singida Motel usiku huu
Rich
Mavoco akiwaimbisha mashabiki wake waliofika kwenye tamasha la Serengeti
Fiesta usiku huu,ambapo wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi
kuwashuhudia wasanii mbalimbali wanaotumbuiza kwenye tamasha hili.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya,Shillole akijimwaya mwaya jukwaa mbele ya
umati wa wakazi wa mji wa Singida (hawapo pichani),usiku huu.
Pichani
juu na chini Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kwa wingi usiku huu
kwenye viwanja vya Singida Motel ambako tamasha la Serengeti Fiesta 2012
likiendelea.
Pichani kati ni msanii wa bongofleva kutoka THT,Recho akiwa sambamba na dansaz wake jukwaani wakikamua vilivyo.
Baadhi ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta wakishangilia jambo.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya,Mabeste na msanii mwenzake wakitumbuiza jukwaani usiku huu
Pichani
ni Ofisa Mahusiano wa kampuni Clouds Fm,Simalenga akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Singida Mjini,Mh Queen Mlozi pamoja na nduguze wakishuhudia
tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu kwenye viwanja vya
Singida Motel,Mkoani Singida ambapo wakazi wa mji huo wameitikia wito wa
kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia wasanii mbalimbali wa muziki wa
kizazi kipya
Anaitwa Ben Paul mmoja wa wasanii mahiri wa Bongofleva katika miondoko ya R&B
Shillole akiwapa dole mashabiki wake waliokuwa wakimshangilia kwa nguvu.
Pichani
kulia ni Dj Zero akiwa amepozi mtangazaji wa kipindi cha XXL,wote
wafanyakazi wa Clouds FM wakishoo love usiku huu kwenye tamasha la
Serengeti Fiesta 2012 ndani ya viwanja vya Singida Motel.
No comments:
Post a Comment