Gari hilo baada ya kushika moto.
Dereva wa hiace hiyo akijaribu kuzima moto.
Baadhi ya abiria waliokuwa ndani ya Hiace wakishuhudia moto huo ukizimwa.
ABIRIA na
dereva wa gari aina ya Toyota Hiace yenye namba za usajili T224 ADZ
inayofanya safari zake kati ya mjini Morogoro na Bigwa, leo mchana
wamenusurika kuungua kwa moto baada ya gari hilo kushika moto eneo la
mlima wa Kwa Mnyonge jirani na kiwanda cha mifuko ya nailoni cha Ladwa.
Moto huo
ulizimwa na Wasamaria Wema kufuatia tukio hilo ambapo dereva aliwahi
kuzivua nguo zake zilizokuwa zimeanza kushika moto ulioanzia kwenye
injini. Dereva huyo hakupata madhara yoyote.
No comments:
Post a Comment