Hoteli ya Singita Grumeti Reserves.
HOTELI ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.
Singita
ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa
pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na
taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
Hoteli
hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana
mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji
wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Matokeo
hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha
matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo
linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu
kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi,
matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari,
vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa
mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa
hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma
zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani
(Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa
kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa
kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais,
matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni
na kadhalika.
HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais
wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa
nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa
zake zinazotikisa duniani.
Bilionea
wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich,
alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye
hoteli hiyo.
Bilionea
wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani,
alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati
alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya
mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya
19.
Mke
wa zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole,
Cheryl, alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba
alifikia kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo
aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie
na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi
yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine
ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa
Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya
Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata
hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno,
tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa
hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za
kiusalama.
SIFA ZA HOTELI HIYO
Ni hoteli yenye eneo kubwa, kutoka ‘loji’ moja hadi nyingine, inabidi utumie usafiri maalum.
Imegawanywa kwenye ‘loji’ mbili, moja inaitwa Ebony na nyingine ni Boulder.
Hoteli
hiyo, pia inaundwa na ‘loji’ nyingine inayoitwa Castleton Camp ambayo
inaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Bei ya chini kabisa kwa mtu kulala kwenye hoteli hiyo ni shilingi 2,000,000 na bei hiyo hutegemea na msimu.
Bei
zimetofautiana kati ya ‘loji’ moja hadi nyingine na mtu kulala kwenye
Castleton Camp, inaweza kugharimu mpaka shilingi milioni 23 kwa siku
moja.
Singita Grumeti ni moja kati ya hoteli za Singita za nchini Afrika Kusini.
Habari kwa hisani ya GPL
No comments:
Post a Comment