Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 20, 2012

JUST IN: Rufaa ya Lema imeahirishwa hadi Oktoba 2, 2012; uwezekano mkubwa hukumu kusomwa Dar es Salaam




DSCN5261
Shauri lililofunguliwa na aliekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaaa nchini kupinga kuenguliwa kwake kuwa mbunge limeahirishwa hadi tarehe 2 mwezi ujao litakaposikilizwa tena.


Mapema asubuhi ya leo mamia ya wafuasi wa Chadema walijitokeza katika eneo la Mahakama Kuu kusikiliza rufaa hiyo ambayo ilisikilizwa kwa muda mrefu kiasi kabla ya kuahirishwa.

Imeelezwa kuwa, upande wa walalamikaji wameweka mapingamizi fulani ambayo jopo la majaji litayapitia hiyo tarehe 2 oktoba.

Taarifa nyingine ambayo haijaweza kuthibitishwa na Blog hii zinaeleza kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa hukumu ya rufaa hii kusomwa Dar es Salaam.
Kwa hisani ya Arusha 255 blog

No comments:

Post a Comment