MMOJA YA NYUMBA KATIKA ENEO LA TANA RIVER.
NYUMBA 20 zimeteketezwa moto leo asubuhi na watu wasiojulikana katika eneo la Tana River nchini Kenya ambako kumekuwa na mapigano ya kulipiza kisasi katika siku za hivi karibuni kati ya jamii zinazoishi huko.
Kufuatia tukio hilo polisi wamewakamata watu 19 huku wakiendelea na harakati za kuwapokonywa wananchi silaha.
Ripoti kutoka katika eneo Tana Delta zinaarifu kuwa tukio hilo la
kutetekeza nyumba lilitekelezwa saa kumi na mbili asubuhi na watu
wasiojulikana katika vijini vya Ozi, Kipini na Bura.
Hatua hii inajiri wakati maafisa wa polisi wameanza shughuli ya kuwapokonya silaha ndogo ndogo waakazi wa maeneo hayo.
Katika msako wa leo asubuhi, bunduki mbili zilipatikana miongoni mwa wakaazi wa maeneo hayo.
Maafisa wa usalama katika eneo hilo walitoa amri
kwa wenyeji kurejesha silaha ndogo wanazomiliki na ambazo wamekuwa
wakitumia kwa mashambulizi ya wenyewe kwa wenyewe.
Hata hivyo kwa kuwa uhasama kati ya jamii hizi
umekuwa ukiendelea kwa muda mrefu baadhi wanahofia ikiwa kweli hatua ya
kuwataka wenyeji kurejesha silaha huenda ikamaliza tatizo la silaha
zilizozagaa miongoni mwa wenyeji wa eneo hilo, ikizingatiwa kuwa hofu
ingali imetanda miongoni mwa wenyeji kufuatia machafuko yaliyosababisha
vifo vya zaidi ya watu 100.
Na pia inahofiwa ikiwa kweli tatizo la silaha au la.
Wadadisi wanasema kuwa japokuwa serikali
imechelewa kuchukua hatua ili kuzima ghasia za Tana River, inatikiwa
kufanya utafiti zaidi kabla ya kutekeleza mipango hiyo ili kuweza
kukadiria ufanisi wake inapojihusisha na shughuli kama hiyo.
Serikali ya Kenya ilivituma vikosi zaidi vya polisi katika eneo hilo ambalo linakaliwa na jamii za wa Orma na wapokomo.
Kadhalika bunge la Kenya lilipitisha hoja ya
kuwapeleka wanajeshi katika eneo hilo kwa minajili ya kuzidhibiti jamii
hizo zinazozozana hasa baada ya polisi kuonekana kushindwa nguvu . Mzozo
katika eneo la Tana Delta umehusishwa na tofauti za kisiasa, maji na
malisho ya mifugo miongoni mwa maswala mengine.
You might also like:
No comments:
Post a Comment