Brandts kulia akiwa na Saintfiet wakati wa Kagame |
BEKI
wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi na klabu ya PSV Eindhoven ya
Holanzi, Ernstus ‘Ernie’ Wilhelmus Johannes Brandts, ndiye kocha mpya wa
Yanga na atawasili wakati wowote kuanzia kesho kusaini mkataba na
kuanza kazi.
Mholanzi
huyo aliyefukuzwa APR ya Rwanda baada ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki
na Kati, Kombe la Kagame, Agosti mwaka huu amepewa ukocha wa Yanga,
baada ya Mbrazil Marcio Maximo kukataa nafasi hiyo kwa mara ya pili.
Mtaalamu
huyo, alizaliwa Februari 3, mwaka 1956 mjini Nieuw-Dijk, Gelderland,
mbali na PSV Eindhoven, alichezea pia Roda JC Kerkrade, MVV Maastricht
na De Graafschap.
No comments:
Post a Comment