Mwenyekiti
wa Jumuiya ya Madaktari walioathirika na mgomo Dr. Paul Swakala
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
…………………………………………………….
MADAKTARI
wanaofanyakazi chini ya usimamizi wa madaktari bingwa (Interns),
hatimaye wamejitokeza na kuwaomba radhi wananchi pamoja na serikali
kutokana na kitendo chao cha kufanya mgomo ambao umesababisha madhara
kwa baadhi ya wananchi.
Wakizungumza
na wandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo),
Kiongozi wa Madaktari hao, Dk Paul Swakala, alisema mtakumbuka kuwa
Juni mwaka huu ulitokea mgomo wa madaktari ukiwa ni mwendelezo wa mgomo
uliyoanza Desemba 2011.
Alisema
wanawaomba radhi Wananchi wenzao na serikali kutokana na madhara yote
yaliyosababishwa na migomo ile ambayo ushiriki wao ulikuwa hauepukiki.
Dk
Swakala alisema kuwa wapo walioathirika na mgomo ule, wanaomba radhi
pamoja na usumbufu huo ambapo wanakiri pia kuwa wananchi wengi
walichukizwa na migomo hiyo.
“Ingawa
utamaduni wa kuomba radhi hadharani katika nchi yetu haujazoeleka
lakini tumeamua kufanya hivyo kwa sababu sisi ni binadamu na binadamu
wote tunamapungufu.
“Pia
tunamuomba radhi Rais Jakaya Kikwete na serikali yake kwa usumbufu
uliosababishwa na mgomo ule ambapo tunatambua jitihada zake za kutafuta
suluhu ya mgomo ule”alisema.endelea kupitia audiface jackson blogspot kwa habari zaidi..Vilevile
wanatambua na kuunga mkono juhudi zake katika kuboresha huduma za afya
nchini na changamoto nyingi ambazo zinaikabili sekta hiyo nchini.
Hata
hivyo, alisema wanazidi kumuomba aiangalie zaidi sekta hiyo kwani
maisha ya Watanzania wengi wanategemea huduma bora za sekta hiyo.
Alisema
wanawahakikishia watanzania kuwa hawako tayari tena kushiriki kwa namna
yeyote katika migomo inayoweka rehani maisha ya wananchi.
“Kwa
hakika, tunajutia sana kosa hili na tuko tayari kurejea kazini
kuendelea kuwahudumia watanzania wenzetu kwa moyo mweupe”alisema
Kama hiyo haitoshi, wanayo dhamira ya kweli ya kuomba kuonana na Rais ili waweze kuomba radhi kwake ana kwa ana.
No comments:
Post a Comment