Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Anna
Maembe (wa kwanza kulia) akijiandikisha kushiriki mkutano wa 14 wa
Mawaziri wa Mazingira barani Afrika ambao unazinduliwa leo jijini Arusha
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari Nkoanrua ya wilayani Arumeru ambao ni wadau wa
Mazingira shuleni hapo kwa kushirikiana na YVE Tanzania wakisubiri
kushiriki Mkutano wa Mazingira leo jijini Arusha.
Mwakilishi wa MO BLOG Bw. Mahmoud Ahmad akizungumza na wanafunzi sekondari Nkoanrua ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha.
Wageni watakaoshiriki mkutano wa mazingira wakiperuzi mitandao katika ukumbi wa mikutano wa AICC.
Wadau kutoka NEMC wakijadiliana jambo.
Wataalam
kutoka mtandao wa mazingira ulio chini ya NEMC ambao utazinduliwa leo
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal.
Pichani Kulia ni Dkt. Christopher Muhando na kushoto ni Bw. Obadia
Machupa.
Wadau kutoka NEMC wakiaanda sehemu yao ya kutoa maelezo kwa wadau mbalimbali wa mazingira kutoka nchi 53 za Afrika.
Mtaalamu wa Mazingira kutoka Gabon Bi. Marie Rosine Itsana.
Pichani ni Wawakilishi kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Mtaalamu wa Mazingira na Nishati wa UNDP Dkt. Amani Ngusaro.
Vodacom
nao wapo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wageni wanaohudhuria
mkutano wa 14 wa Mazingira barani Afrika unaozinduliwa rasmi leo mchana
na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment