Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 23, 2012

MATUKIO YOTE YANGA VS JKT, MTIBWA YATOTA CHAMAZI



Wachezaji wa Yanga, wakimpongeza Kavumbangu baada ya kufunga bao la pili

Cannavaro anafunga bao la kwanza

Kiiza na Kavumbangu wakimpongeza Cannavaro
  
Chuji akimuelekeza Niyonzima namna ya kupiga mpira wa adhabu uliozaa bao la kwanza 
DUWA LA KUKU; Wachezaji wa JKT wakiomba dua kabla ya mechi

Kikosi cha JKT leo

Kavumbangu akishangilia bao la nne

Makocha wa Yanga, Freddy Minziro (kulia) na Mfaume Athumani 

Mwenyekiti wa Yanga, akitoka kwenye chumba cha wachezaji wakati wa mapumziko

Msuva anafanya safari
Msuva hatari sana 
Shamte Ally anamtoka mtu 
Shamte anashughulika
Wakubwa wakijipanga kwa kazi
11 wa Yanga walioanza leo

YANGA SC jioni hii imepata ushindi wa kwanza ndani ya mechi tatu za Ligi Kuu ya 
Vodacom Tanzania Bara, baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 4-1 kwenye Uwanja wa 
Taifa, Dar es Salaam.
Hadi mapumziko Yanga walikuwa tayari mbele kwa mabao 2-0, yaliyotiwa kimiani 
na Nahodha, Nadir Haroub Ally ‘Cannavaro’ dakika ya nne na Didier Kavumbangu
 dakika ya 31, mabao yote yakitokana na kazi nzuri ya kiungo mshambuliaji Simon 
Msuva.
Bao la kwanza ulikuwa mpira wa adhabu uliopigwa na Haruna Niyonzima, baada ya 
Msuva kuangushwa karibu kabisa na eneo la hatari la JKT Ruvu na bao la pili dogo
 huyo aliyesajiliwa kutoka Moro United iliyoshuka daraja, alimpa pasi mshambuliaji
 wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu.
Kipindi cha pili, Yanga walirudi tena kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la tatu 
dakika ya 52, mfungaji Simon Msuva kabla ya Didier Kavumbangu kufunga la nne 
dakika ya 65.
JKT ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 68 mfungaji Credo Mwaipopo.
Katika mchezo wa leo, Yanga ilicheza vizuri, wachezaji wakionana kwa pasi nzuri 
ndefu na fupi, tofauti na ilivyokuwa kwenye iliyopita mjini Morogoro, ambako 
walifungwa 3-0 na Mtibwa Sugar.
Ikumbukwe mechi ya kwanza, Yanga ililazimishwa sare ya bila kufungana na 
Prisons mjini Mbeya.
Yanga leo ilicheza chini ya kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro, baada ya 
aliyekuwa Kocha Mkuu, Mbelgiji Tom Saintfiet kusitishiwa mkataba jana usiku,
kufuatia kutofautiana na uongozi.
Yanga SC; Yaw Berko, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, 
Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Nizar Khalfan/Shamte Ally, Haruna 
Niyonzima, Didier Kavumbangu/Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Simon Msuva.
JKT; Said Mohamed, Kessy Mapande, Stanley Nkomola, Damas Makwaya, Charles 
Timoth, Ally Khan, Haroun Adolf, Said Ahmed ‘Ortega’/Jimmy Shoji, Omar 
Changa/Furaha Tembo, Hussein Bunu na Sosstenes Manyasi/Credo Mwaipopo.
Kwenye Uwanja wa Chamazi, wenyeji Azam FC wameifunga Mtibwa Sugar 1-0,
 bao pekee la Kipre Herman Tchetche, wakati Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
 Arusha wenyeji JKT Oljoro 1-0 wameifunga Polisi Morogoro, bao pekee la Paul 
Ndonga dakika ya 13 na  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wenyeji Coastal Union wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Toto Africans.source bin zubeiry

No comments:

Post a Comment