Mtambo
wa kuchimbia madini ambao Raia wa China walikamatwa wakiutumia katika
pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkansi kinyume cha sheria.Raia huyu wa
china amehukumiwa kulipa faini na kuamriwa kuondoa mtambo huo katika
pori hilo.
Baadhi
ya raia wa China na Watanzania wakishirikiana kuchimba madini katika
pori la Akiba la Lwafi,wilayani Nkansi kinyume cha sheria,ambapo raia
hao wa china walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa kulipa faini.(Picha/
Tabu Ndziku)
NA VERONICA KAZIMOTO-MAELEZO
Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa Kampuni ya REDore Mining mwenye asili ya Asia Chaoxian Zhou
amehukumiwa kwenda jela miaka minne au kulipa faini jumla ya Shilingi
1,350,000/= kwa kukutwa na makosa mbalimbali likiwemo lakuchimba madini
ndani ya hifadhi ya Pori la Akiba la Lwafi wilayani Nkasi kinyume cha
sheria .
Kwa
mujibu wa taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wanyama pori Paul
Sarakikya, mtuhumiwa amelipa faini na kuachiwa huru.Makosa megine
aliyopatikana nayo ni pamoja na kuingia ndani ya Pori la Akiba Lwafi
kinyume na Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na 5 ya mwaka 2009 kifungu
cha 15 na kuharibu mimea ndani ya Pori la Akiba kwa kukiuka kifungu cha
18 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori.
Makosa
mengine ni pamoja na kuchimba madini ndani ya Pori la Akiba bila kibali
kinyume na Kifungu cha 20 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori na
kuchimba madini ndani ya hifadhi kinyume na kifungu cha 95(1) (c) cha
Sheria ya madini Na. 14 ya mwaka 2010.
Mshtakiwa
alikiri makosa yote mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Mpanda
mkoani Katavi Richard Kasele na Mwendesha Mashtaka Bwana Prosper
Rwegerera na kupatikana na hatia ya kuchimba madini katika eneo la
Kanyamakaa lililoko katika Wilaya ya Nkasi kinyume cha sheria ya
Kuhifadhi wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009.
Taarifa
hiyo imefafanua kuwa mshitakiwa ameamriwa kuondoa mitambo iliyokutwa
ndani ya Pori la Akiba la Lwafi na kufukia mashimo na mitaro yote
iliyochimbwa kutokana na shughuli za Kampuni hiyo ndani ya siku saba.
Aidha Madini yaliyokuwa yamechimbwa katika eneo hilo ambayo thamani yake
bado haijajulikana yametaifishwa na Serikali.
Chaoxian
Zhou na mwenzake Wei Lyu ambao wote ni raia wa China walikamtwa Julai
25, 2012 ambapo iligundulika kuwa Wei Lyu hakuwahi kwenda mkoani Katavi
wala katika Hifadhi hiyo ya Lwafi na kuchimba madini hivyo aliachiwa
huru
You might also like:
No comments:
Post a Comment