Mgomo
uliokumba mojawapo ya migodi nchini Afrika Kusini wa dhahabu ,AngloGold
Ashanti, sasa umeenea hadi katika migodi mingine ya kampuni hiyo nchini
humo.
AngloGold
imesema kuwa wengi wa wafanyakazi wake, takriban 35,000 nchini humo,
wanashiriki katika migomo hiyo wakidai nyongeza ya mishahara.
Takriban
watu 46 waliuawa wakati wa maandamano ya kudai nyongeza ya mishahara
katika mgodi wa Marikana.Mgomo huu unajiri baada ya wafanyakazi wa
kampuni ya madini ya Lonmin kurejea kazini wiki jana baada ya kugoma
vile vile wakitaka mishahara mizuri.
Uchunguzi wa mauaji hayo utaanza tarehe moja mwezi ujao.
Mgomo mwingine ambao hauhusiani na huu wa AngloGold, unaendelea katika mgodi mwingine wa dhahabu wa Gold Fields.
Mgomo huu
wa AngloGold ulianza wiki jana katika mgodi wa Kopanang na kuenea hadi
katika mgodi wa Mponeng ambao ndio wenye uketo mkubwa zaidi duniani.
No comments:
Post a Comment