Msanii
wa Kundi la Vichekesho, Mkwere kutoka kundi la Mizengwe akiigiza kama
Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa
burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo
mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo
Septemba 17-22, 2012. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”
Mgeni
rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na
Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed
Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.
Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa
Meneja
Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi
Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi
wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini
wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine
katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza
la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa
Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri
wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi, akimkabidhi cheti cha heshima
kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza ajali
barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, Meneja wa Airtel
Kanda za Nyanda za Juu Kusini, Beda Kinunda.Makabidhiano hayo
yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa
mkoani Iringa.
Mkurugenzi
Mkuu wa Makampuni ya ASAS, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wiki
ya Nenda kwa Usalama Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed, akipokea cheti cha
heshima kwa kuwa wachangiaji katika kampeni ya kupambana na kupunguza
ajali barabarani pamoja na Wiki ya Nenda kwa Usalama kitaifa, kutoka kwa
Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel
Nchimbi. endelea kupitia audiface jackson blogspot kupata habari zaidiMakabidhiano hayo yalifanyika jana katika ufunguzi wa Wiki ya
Nenda kwa Usalama Kitaifa mkoani Iringa.Picha Kwa Hisani Ya Father Kidevu Blogu
No comments:
Post a Comment