Mtikila akijiandaa kwenda kusikiliza kesi yake.
Mzee wa kesi akiwa ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
Mtikila akisubiri muda wa hukumu ufike.
Mchungaji mtikila akipata habari kidogo
Furaha ya ushindi dhidi ya serikali
Akiongea na waandishi wa habari waliojitokeza mahakamani hapo.
Kila mmoja akihangaika huku na kule kupata taswira nzuri..
Mtikila
amkimsikiliza Koplo wa Polisi mwenye RB Namba : KMR/RB/10482 yenye
maelezo ya kutishia kuuwa kwa maneno na wizi wa viwanja iliyofunguliwa
na bwana Gotta Ndungulu.
Mtikila
akitoa onyo kali kwa Polisi mwenye cheo cha Koplo kwa kutaka kumkamata
kwa madai kuwa yeye ni kiongozi wa Kitaifa na mwenye uwezo wa kumkamata
ni mwenye ofisa wa Polisi mwenye cheo cha juu.
Mtikila akiondoka Mahakamani baada ya kushinda kesi na kutokamatwa na polisi.
MWENYEKITI
wa Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila, leo ameshinda
hukumu ya kesi yake iliyokuwa inamkabili. Mtikila ameshinda katika kesi
hiyo iliyokuwa ikisikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele
ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Elivin Mgeta. Mtikila alikuwa
anakabiliwa na tuhuma za uchochezi dhidi ya serikali na kukutwa na
nyaraka za uchochezi.
No comments:
Post a Comment