Naibu
waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge (kushoto) akitoa maelekezo kwa
mkandarasi anayejenga barabara inayopita eneo la Jangwani,Kigogo na
kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha ubungo yenye urefu wa km
6.4 Injinia Abdul Kimaro (kulia kwa naibu waziri) leo wakati wa ziara
ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara jijini
Dar es salaam.
Mhandisi
wa Miradi kutoka wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Ntije Nkolante
(kulia) akimwonyesha Naibu Waziri wa Ujenzi Gerson Lwenge (aliyenyosha
mkono kushoto) sehemu ya mwinuko ambayo iko kwenye matengenezo katika
barabara iendayo Yombo Vituka yenye urefu wa kilometa 10.3 inayojengwa
na kampuni ya Nyanza Roads Work leo jijini Dar es salaam.
Sehemu
ya barabara ya Yombo Vituka ambayo ujenzi wake umekamilika yenye urefu
wa kilometa 10.3 inayojengwa na kampuni ya Nyanza Roads Work jijini Dar
es salaam.
No comments:
Post a Comment