Angel Gasper (19)
Na Princess Asia
SHINDANO la
kumsaka mlimbwende wa Kanda ya Temeke, Miss Temeke 2012 linafanyika leo katika
ukumbi wa PTA, Sabasaba, Dar es Salaam na mshindi atazawadiwa Sh. Milioni 1.5 mbali
na tiketi ya kushiriki Miss Tanzania baadaye mwaka huu.
Benny
Kisaka, Mkurugenzi wa BMP Promotions, waandaaji wa Miss Temeke 2012, aliiambia BIN
ZUBEIRY jana kwamba, katika mlolongo huo wa zawadi, mshindi wa kwanza
atajinyakulia fedha taslim Sh. Milioni 1.5, wa pili Sh. 800,000, wa tatu Sh. 700,00
sambamba nguo ya kutokea jioni na viatu, vyenye thamani ya Sh. 500,000 kila
mmoja kwa wote watatu.
Kisaka
alisema kwamba duka la kisasa la Mariedo Boutique itatoa gauni la Sh.350,000 na
kiatu cha Sh 150,000 kila mmoja kwa washindi hao watatu wa kwanza
watakaoshinda. Alisema mbali ya washindi hao, mshindi wa nne atajinyakulia
kitita cha Sh. 400,000 ambapo mshindi wa tano
ataondoka na Sh 300,000 wakati warembo wengine wote watakaosalia kila
mmoja atapata Sh.200.000.
Ikiwa ni
funga dimba ya mashindano ya urembo ya kanda nchini, shindano hilo litanogeshwa
na wasanii wanaong’ara katika luninga, Mpoki wa kundi la Orijino Komedi na Steve Nyerere ambaye mbali ya kuigiza sauti
za watu mbalimbali, pia ametoa filamu kadhaa kwa siku za hivi karibuni.
Mbali ya
wasanii hao, bendi ya Mashujaa Musica, yenye wanamuziki nyota kama Charles
Baba, MCD, Ferguson, Ali Akida na wanennguaji kama Lillian Internet na wengineo
pia itanogesha usiku huo.
Taji la Miss
Temeke, linashikiliwa na Husna Twalib na washiriki walikuwa wakijifua kwa wiki
tatu chini ya mkufunzi, Leilla Bhanji, ambaye amekuwa akisaidiwa pia na warembo
wa miaka ya nyuma wa Miss Temeke akiwemo, Regina Mosha (2002, Hawa Ismail 2003),
washiriki wa mwaka jana Joyce Maweda, Mwajabu Juma, Cynthia Kimasha na katika
shoo wamekuwa na Dickson Daud kutoka kundi la THT.
Shoo ya
ufunguzi itakuwa tofauti kabisa na shoo nyingine yeyote iliyowahi kuyanyika
nchini, kwani imezingatia zaidi urembo na nini msichana anatakiwa kufanya na si
unenguaji tu. Warembo 15 wanatoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na
Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa
kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012.
Warembo hao
ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine
Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph,
Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam
Ntakisivya na Esther Albert.
Temeke inajivunia
kutwaa taji la Miss Tanzania mara tatu, kupitia warembo Happiness Sosthenes Millene
Magesse mwaka 2001, Sylvia Remmy Bahame mwaka 2003 na Genevieve Mpangala mwaka 2010.
Lakini pia
imetoa warembo waliowahi kushika nafasi ya pili na tano bora katika Miss
Tanzania kama Jokate Mwegelo, Irene Uwoya, Irene Kiwia, Queen David, Cecylia
Assey, Sabrina Slim, Miriam Odemba, Ediltruda Kalikawe na Asela Magaka. |
No comments:
Post a Comment