Meneja
wa TANESCO mkoa wa Singida Maclean Mbonile akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo kwenye picha) juu ya mkakati wa uboreshaji wa huduma za
shirika hilo. (Picha na Nathaniel Limu).
Meneja
wa shirika la TANESCO mkoani Singida Maclean Mbonile amewaomba
waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuhamsisha wananchi washiriki
kutoa maoni yao yatakayosaidia uboreshaji wa huduma za TANESCO ili
ziweze kukidhi mahitaji ya wateja.
Meneja
Mbonile ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza na waandishi wa
habari ofisini kwake, juu ya mchakato wa kufanya mabadiliko ya kimuundo
na kiutendaji kwa lengo la kuboresha huduma za TANESCO.
Akifafanua,
amesema shirika la TANESCO linakusudia kufanya mabadiliko makubwa ya
uboreshaji wa huduma zake, ili shirika liweze kutekeleza majukumu yake
ya kuwahudumia wateja wake kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Amesema
ili uboreshaji huo wa huduma uweze kufanikiwa kwa kiwango cha juu,
wananchi na wateja hawana budi kushiriki kutoa maoni yao juu ya TANESCO
mpya iweje.
Aidha,
amesema kila mtoaji wa maoni hayo, anatakiwa kuandika namba yake ya
simu, ili endapo ufafanuzi zaidi utahitajika, mhusika aweze kupatikana
kwa urahisi.
Katika hatua nyingine, Mbonile amewataka waandishi wa habari kushirikiana na TANESCO katika mapambano dhidi ya wezi wa umeme.
Amesema asilimia 30 ya umeme wa TANESCO, unaibwa na wahalifu kwa njia ya kujiunganishia umeme na wengine kuchezea mita.
No comments:
Post a Comment