Mwenyekiti
wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof.Ibrahim Lipumba akiwasili kwenye
Mkutano wa Chama hicho uliofanyika Jangwani jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wananchi na wanachama wa chama hicho waliojitokeza kwenye mkutano huo.
Wafuasi wa Chama hicho wakifurahia jambo.
Kikundi cha Mchiriku nacho hakikua mbali kutumbuiza.
Kadi za vyama mbalimbali zilirejeshwa na kukabidhiwa kadi mpya.
Afande Sele nae alitumbuiza kwenye mkutano huo.
Msanii
Kala Pina, akitoa burudani kwa wanachama wenzake wa chama hicho, kwenye
uchaguzi wa 2010, Kalapina aligombea udiwani kupitia chama hicho kwenye
kata ya Kinondoni.
KATIKA
kile kinachoonekana ni kujipanga kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwaka 2015, Chama cha wananchi CUF leo kimezindua mkakati mpya wa
kujiimarisha nchi nzima.
Akiwahutubia
maelfu ya wanachama waliohudhuria kwenye mkutano mkubwa Mwenyekiti wa
chama hicho Prof. Ibrahim Lipumba pamoja na mabo mengine ya kiuchumi wa
dunia na wa hapa nchini lakini hakuacha kugusia mkakati wa chama hicho
kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015.
Alisema
chama chake kimejipanga kimkakati kuelekea uchaguzi huo na anaamini
watanzania watakiunga mkono kwani ni ndio chama pekee chenye sera
mbadala za kuleta mabadiliko. Aidha Prof. Lipumba alisema uchumi wa
dunia kwasasa uko katika halimbaya sana lakini hali mbaya hiyo inatoa
fursa kwa nchi masikini kujiimarisha kupitia kilimo kutokana na bei ya
mazao ya kilimo kuongezeka duniani kote.
Aidha
Lipumba alifafanua kuwa kuongezeka kwa mahitaji ya mazao ya kilimo
kunatokana pia na kuimarika kwa uchumi kwenye nchi ambazo zina watu
wengi akitoa mfano wa China na India ambazo zinawatu zaidi ya bilioni
moja .
Awali
akizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye mkutano huo Naibu
Mkurugenzi wa habari na uenezi wa Chama hicho Abdull Kambaya, alisema
tabia ya chadema ya kuisema CUF kama ni CCM B, ni yakuficha ukweli
kwamba wao ndio CCM B kwa kuendesha chama chao chini ya misaada ya
makada wa CCM akiwamo kada maarufu wa chama hicho Mustafa Sabodo. Hata
hivyo akahoji kuwa kitendo cha chama hicho kwenda kuombaomba CCM kupata
wagombea ni kitendo cha kutojiamini.Picha/Habari Kwa Hisani ya Burudani
Mwanzo
No comments:
Post a Comment