Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, September 27, 2012

UTENDAJI MBOVU NI CHANZO CHA KUZOROTA KWA HUDUMA PANTONI ZA KIGAMBONI



UTENDAJI kazi usiyofuata  kanuni katika pantoni za Serikali Kigamboni, umeelezwa kuwa ndiyo chanzo cha kuzorota huduma na kusababisha usumbufu kwa wananchi wanaotaka kuvuka nyakati za asubuhi. 
 wakazi hao walisema pale Feri kumekuwa na miungu watu wanaofanyakazi wanavyotaka bila kujali haki za watu wengine.
Walisema utakuta wafanyakazi hao wa pantoni hizo kwa makusudi huamua kufanyakazi kwa kutumia pantoni moja baadala ya vyote viwili kitendo ambacho husababisha msongamano wa biria na magari.
Mmoja wa wakazi wa Kigamboni, Daina Christopher,  alisema usumbufu wanaoupata kutoka kwa wafanyakazi wa vivuko hivyo unawafanya hadi baadhi ya watu wengine kufikiria kuhamia mjini.
“Mimi nashangaa sana kwani utakuta wafanyakazi hao  kwa utashi wao wenyewe wanaamua kupunzisha pantoni moja eti wakidai kuwa wanabana gharama za mafuta kitendo ambacho hakieleweki”alisema Daina.
Alisema kama serikali imewaagiza hivyo kutumia kivuko kimoja basi itambuwe kuwa haiwatendei haki kwa kuwa utaratibu huo umekuwa ukisababisha usumbufu kwa wananchi kuchelewe katika majukumu yao ya uzalishaji kipato.
Naye Khamisi Halid hapendezwi na utaratibu unaofanywa na wafanyakazi katika pantoni hizo pale wanapotumia mashine mbili huku nyingine mbili zikizimwa kwa makusudi ili mafuta yake wayachukuwe kwa maslahi yao binafsi.
Alisema wafanyakazi hao wamekuwa wakifanya hujuma mbalimbali lakini cha kushangaza hata wanapopiga kelele kwenye vyombo vya habari hakuna hatua za uwajibishaji zinazotekelezwa.Endelea kupitia audifacejackson blogspot..“Mwandishi naona unajisumbua kwani wewe siyo wa kwanza, wamekuaja wengi na tumewaeleza kama haya lakini bado wanatutesa haiwezekani pantoni ziko mbili lakini kwa makusudi wanaamua kutumia moja ili mradi waibe mafuta sasa sisi tunawaachia nyinyi vyombo vya habari”alisema.
Fullshangweblog  ilipouliza kuhusu madai hayo kwa baadhi ya wafanyakazi wa pantoni hizo kila moja aliruka wakidai kuwa wao si wasemaji.
“Pamoja na kuwa sisi siyo wasemaji lakini madai hayo yanalengo la kutuharibia kazi zetu”alisikika mmoja wawafanyakazi hao akisema bila kutoa ufafanunuzi kuhusu ucheleweshaji wa kuwavusha wananchi huku akikataa kutaja jina lake.

No comments:

Post a Comment