Sanga akizungumza na Waandishi wa Habari mida hi. kulia ni Tito Osoro, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na kushoto Isaac Chanji, Mjumbe wa kuteuliwa |
Na Mahmoud Zubeiry
UONGOZI wa
klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, umeisimamisha kazi Sekretarieti nzima ya
klabu, akiwemo Katibu Celestine Mwesigwa na Ofisa Habari, Louis Sendeu,
kutokana na kile ilichoeleza utendaji usioridhisha.
Akizungumza na
Waandishi wa Habari ‘mida hii’ makao
makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement
Sanga alisema kwamba maamuzi hayo yamefuatia kikao cha Kamati ya Utendaji
kilichofanyika tangu saa 5:30 leo hadi saa 9:30.
Wengine wanaokumbwa
na panga hilo ni Masoud Saad, aliyekuwa Ofisa Utawala, Philip Chifuka aliyekuwa
Mhasibu na Hafidh Saleh aliyekuwa Meneja ambaye anahamishiwa kwenye majukumu
mengine.
“Tumesitisha
mikataba ya sekretarieti nzima, pia tumefanya marekebisho, tumemtoa Meneja wa
timu na muda si mrefu tutamtangaza Meneja mwingie pamoja na sekretarieti mpya,”alisema
Sanga.
Aidha, Sanga
alisema Kocha Mbelgiji, Tom Saintfieti anapewa onyo kali kwa kuzungumza ovyo na
vyombo vya habari.
“Tumekwishakutana
naye mara kadhaa kumpa utaratibu wa kuzungumza na vyombo vya habari, sasa tutamuandikia
barua ya kumkumbusha wajibu wake na kuzingatia wajibu wake, kutozungumza na
vyombo vya habari holela,”alisema.
Kwa ujumla
maamuzi haya yanakuja baada ya Yanga kuanza vibaya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
Bara, ikiambulia pointi moja tu katika mechi zake mbili za awali, kutokana na
sare ya bila kufungana na Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Jumamosi
na Jumatano ikachapwa mabao 3-0 Morogoro Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
No comments:
Post a Comment