Nyota
wa kandanda katika ligi ya soka ya Ujerumani inayofahamika kama
Bendesliga, Michael Ballack (pichani) ametangaza rasmi kustaafu
kandanda.
Ballack
ametoa taarifa hiyo kupitia mwanasheria wake, ambapo katika tamko lake,
amekumbushia matukio muhimu kwenye historia ya kazi yake hiyo na kusema
kuwa ataukumbuka mchezo wa soka, lakini mapumziko yake ya mwaka huu
yamemuonyesha kuwa huu ni wakati muafaka kustaafu.
Kiungo huyo wa zamani amesema kwa sasa anasonga mbele kufungua ukurasa mpya wa maisha.
Amewahi kuzichezea timu za Kaiserslauten, Bayern Leverkusen, Bayern Munich na Chelsea.
Michael
Ballack pia amewahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani kwa
miaka kadhaa na kucheza jumla ya michezo 98 na kushinda mabao 42.
No comments:
Post a Comment