ASKARI
polisi hapa nchini wametakiwa kufanyakazi kwa kufuata sheria,
maadili na misingi ya polisi nchini ikiwa ni pamoja na kuepuka
matumizi ya nguvu na silaha za moto katika kutekeleza majukumu yao ili
kuepuka matukio ya kuua raia.
Mkuu wa
jeshi la polisi nchini IGP Saidi Mwema aliyasema hayo wakati akifunga
mafunzo ya uongozi mdogo jeshini katika chuo cha taaluma ya polisi
moshi ambapo alisema suala la ulinzi na usalama katika nchi ni jukumu
la kila mtanzania pasipo kujali nafasi na cheo alicho nacho .
Alisema
polisi wanapaswa kuangalia ulazima na umuhimu wa kutumia nguvu katika
utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na kufuata sheria na kwamba
polisi atakayekwenda kinyume atawajibishwa kwa mujibu wa kanuni na
sheria za jeshi hilo.
Alisema
uwajibikaji wa polisi na wananchi ni jambo la msingi hususani katika
kipindi hichi ambacho jeshi hilo linaupungufu mkubwa wa askari ambapo
askari mmoja analazimika kuhudumia wananchi 1300 badala ya wananchi 400
kama inavyopaswa kidunia
Aidha
alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 89 ya watanzania hawana
ufahamu wa kutosha kuhusiana na suala la ulinzi na usalama na badala
yake wanaamini kuwa jukumu la usalama ni la Polisi na viongozi jambo
ambalo si sahihi.
“Ulinzi
na usalama ni jukumu la kila mmoja na si la polisi wala viongozi
pekee,watanzania wote tuwajibike katika kulinda ulinzi na usalama wa
nchi,na katika hili tutafanikiwa kukomesha matukio ya kiuhalifu na
kuimarisha amani na utuli” alisema Mwema.
Kwa
upande wake kaimu mkuu wa chuo cha taaluma ya polisi Bw.Robert
Boaz alisema jumla ya askari 2825 kati ya 2865 wamefanya vizuri
mitihanai yao na kupandishwa vyeo wakati 41 wamefeli na kutakiwa kurudia
kwa wiki moja na watakao faulu ndio watapandishwa vyeo
Naye kaimu
mkuu wa mkoa wa kilimanjaro Bw..Elinas Palanjo alisema askari
wasijivunie vyeo walivyovipata bali watambue kuwa vyeo hivyo ni
majukumu na wanapaswa kuyatekeleza kwa mujibu wa sheria na taratibu.
No comments:
Post a Comment