Mwanaharakati
wa kisiasa nchini Afrika Kusini, Julius Malema, ameelezea
kughadhabishwa na ripoti kuhusu madai ya ufisadi yanayohusisha kampuni
anayoimiliki.
Alisema
kuwa uchunguzi uliofanywa na mhifadhi wa mali ya umma, Thuli Madonsela
kuhusu kampuni yake kupewa zabuni na serikali , ilimpata na hatia ya
ufisadi bila yeye mwenyewe kuwepo.Bi Madonsela alisema kuwa hatua za
kisheria zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya kampuni hiyo.
Mwezi jana,bwana Malema alikanusha madai ya kujipatia pesa haramu ambazo zilihusishwa na kutolewa kwa zabuni za serikali.
Mwanasiasa
huyo mwenye utata na ambaye amefurushwa kutoka chama tawala, kwa
kuchochea migawanyiko chamani, alisema kuwa kesi hiyo imeshinikizwa
kisiasa.
Katika
ripoti yake, kuhusu kutolewa kwa zabuni za serikali, Bi Madonsela
alidokeza kuwa zabuni ya huduma na usafirishaji wa bidhaa iliyotolewa na
idara ya serikali ya barabara na usafiri katika mkoa wa Limpopo, kwa
kampuni ya uhandisi ya On-Point Engineering, haikuwa halali.
Aliongeza
kuwa Bbwana Malema na mshirika wake wa kibiashara wanaomiliki kampuni
hiyo, walijinufaisha kwa vitendo fisadi vya kampuni yenyewe na idara ya
usafiri ya serikali.
Ripoti
ilisema kuwa kampuni hiyo ilishinda zabuni ya dola milioni 51 mnamo
mwaka 2009 licha ya kwamba ilikuwa imeendesha shughuli zake tu kwa mwezi
mmoja, haikuwa na wafanyakazi wala mali au kupata faida yoyote.
No comments:
Post a Comment