Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrance Mwalusako
WAKATI
klabu ya Yanga ikisisitiza kuendelea kutovaa jezi za wadhamini Wakuu wa
Ligi kuu Bara, kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom, Shirikisho la
soka Tanzania (TFF) litaipiga faini ya shilingi Mil.1.5 timu hiyo
kutokana na kutovaa jezi zenye nembo hiyo.
Yanga
na African Lyon zilivaa jezi isiyo na nembo ya Vodacom zilipomenyana
juzi katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa kwenye dimba la Taifa jijini
Dar es Salaam.
Ofisa
TFF Boniface Wambura alisema kwamba Yanga na Lyon itaadhibiwa kwa
mujibu wa kanuni ya 8 kifungu kidogo cha 38 kintoa adhabu ya faini hiyo
kutokana na kosa hilo.
Alisema
adhabu hiyo ya pia itavikumba vilabu vingine ambavyo vitajaribu kufanya
mambo ambayo yapo kinyume na mkataba wa wadhamini wa ligi hiyo.
Awali,
Katibu Mkuu wa Yanga Lawrance Mwalusako alisema kwamba wataendelea
kuvaa jezi nzisizo na nembo ya Vodacom mpaka pale wadhamini wao
watakapotatua tatizo lao kwani hawako tayari kuvaa kitu chenye doa
jekundu.
Alisema
sakata hilo lilianza tangu msimu uliopita wa ligi hiyo ambapo baada ya
mazungumzo na wahusika walikubalina kuondoa doa hilo kwenye logo
watakayotumia lakini cha kushangaza wameshindwa kufanya hivyo.
“Hatukufanya
makusudi kuvaa jezi tulizopewa na wadhamini bali hatuwezi kuvaa jezi
zenye doa jekundu…sisi tunatumia rangi ya njano, kijani au nyeusi lakini
si nyingine hivyo wahusika inabidi walitatue jambo hilo,”alisema.
No comments:
Post a Comment