Kikosi
cha Young Africans kimewasili salama jijini Arusha jioni hii, na majira
ya saa 12 kimefanya mazoezi mepesi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abed.
Yanga
iliondoka asubuhi leo na basi lao kuelekea jijini Arusha tayari kwa
mchezo wake dhidi ya timu ya JKT Oljoro mchezo utakaofanyika siku ya
jumamosi katika dimba la Uwanja wa Sheikh Amei Abed. yanga imewai kufika
arusha kuzoea hali ya hewa kwa wachezaji na kufanya mazoezi kuuzoea
uwanja wa Sheikh Amei Abed.
katika
kikosi hicho cha wachezaji 20 yanga imeenda na beki wake Kelvin Yondani
wachezaji wengine kwenye msafara huo ni makipa Yaw Berko, Ally Mustafa
‘Barhez’, mabeki, Oscar Joshua, Juma Abdul, David Luhende, Stefano
Mwasyika, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ (Nahodha), Mbuyu TwiteViungo ni
Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Rashid Gumbo, Simon Msuva, Haruna
Niyonzima, Nurdin Bakari, Nizar Khalfan, Juma Seif ‘Kijiko’ na
washambuliaji Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Didier Kavumbangu.
Yanga itacheza na JKT Oljoro siku ya jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom
No comments:
Post a Comment