Bi Pendo akihojiwa na waandishi wa habari |
Bi Pendo Malima (31) mkazi wa Buhare Musoma Mkoani Mara ni
moja kati ya wanawake waliokumbwa na tatizo la domestic violence mkoani humo,
ambapo kutokana na kutokuwa na imani na mawasiliano anayoyafanya kwa kutumia
simu ya mkononi mumewe alimpa kipigo kikali hadi kufikia hatua ya kulazwa
katika hospitali ya mkoa wa Mara huku hali yake ikiwa mbaya na kichwa chake
kinatingishika kutokana na vipigo anavyopata, kisa simu ya mkononi!
Bi Pendo aliwaambia
waandishi wa habari ambao walimtembelea hospitalini hapo kuwa mumewe
anaefahamika kwa jina la Ndege Aloyce humpa kipigo mara kwa mara, lakini
ilifikia hatua akamfungulia dozi ya kipigo yaani mara tatu kwa mwezi hadi
kufikia hatua ya kuzoea dozi hiyo na kuona ni kawaida tu.
Hata hivyo Bi Pendo ambae ni mama wa watoto watatu wa mumewe
huyo anaefanya kazi ya uvuvi alisema atakapopona hatarudi tena kwa mumewe
akiogopa kugeuzwa punching bag. Hii inamaanisha anachotaka kufanya bi Pendo
nikuiacha ndoa yake na kuishi maisha yake bila kurudi kwa mumewe tena pindi tu
atakapotoka hospitalini hapo.
Lakini hii inaonesha kuwa atazidi kunyanyasika kwa sababu
hajui sheria inasema nini na itamsaidia vipi kupata haki yake kutoka kwa mumewe
huyo mgawa dozi ya kipigo. Duh, wanaharakati wa maswala ya kijinsia mna kazi ya
ziada huko Mara na mikoa mingine.
credit kwa Shomari binda blog