Wakati ikiwa zikiwa zimesalia siku mbili kwa wakristo Ulimwenguni
kote kuazimisha siku ya kuzaliwa Bwana na Mwokizi wetu YESU KRISTO siku
ambayo hujulikana kama Christmas, wenyeji wa mikoa ya Kanda ya Kaskazini
hasa Mkoani Kilimkanjaro wanako toka Wachaga na Wapare hii leo
walimiminika kwa wingi katika misafara ya magari madogo binafsi
wakielekea mwakao.
Blogu hii, iliyokuwa njiani ikitoka Arusha ilishuhudia
misafara hiyo ya magari yaliyojaa wanafamilia hao ikifukuzana kuwahi
kupanda safu za milima ya Pare na Uchagani.
Kasi ya Mwaka huu kuongezeka kwa magari madogo barabarani inadaiwa
kuongezeka tofauti na miaka ya nyuma hasa kutokana na kero ya usafiri wa
mabasi na ndege.
Askari wa usalama barabarani nao leo hii walikuwa katika mishe mishe
zao kama kawaida kwa magari hayo mengi kusimamishwa na kufanyiwa ukaguzi
wa hapa na pale na mambo mengine kuendelea.
Jambo kubwa na la kumshukuru Mungu ni kuwa Blog hii katika
pepesa pepesa ya jicho la kamera yake halikufanikiwa kuona ajali yoyote
ya magari hayo wala mabasi zaidi ya magari kadhaa yaliyokutwa yakiwa
yamechemka kutokana na kwenda umbali mrefu.
Walichemka na kuamua nao kufanya mambo.
Magari yaliendelea na msafara
Mvua kidogo ilinyesha barabarani lakini haikuleta madhara
Ni magari ya kila namna yalikuwepo.
Mambo ya namna hii ilikuwepo sana tu.
source father kidevu
No comments:
Post a Comment