Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 28, 2012

Mwanafunzi Amwagiwa Maji ya Moto na mwenzake Wakimgombania Mvulana



Angalia PICHA ....MAZIKO YA SHARO MILIONEA,MAJUTO AKOSA NGUVU KWA MAJONZI,MAMIA WAFURIKA KUMUAGA








 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa mapema mchana huu kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea,Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi mapema mchana huu,Muheza mkoani Tanga.

HII NDIO NDEGE ILIYONUSURIKA KUANGUKA KTK UWANJA WA NDULI IRINGA



Kuna  tetesi  kuwa  ndege  ndogo  iliyokuwa  imewabeba wanafamilia ya Fm Abri Iringa imepata ajali uwanja  wa Nduli Iringa  japo hakuna aliyejeruhiwa  pichani ni ndege  iliyoanguka
Hii  ndio  ndege  iliyonusurika  kuanguka jana katika  uwanja  wa Ndege Nduli mkoani Iringa wakati  ikitua baada ya taili la mbele  kuchomoka .

Hakuna majeruhi  katika ajali  hii japo inasemekama  watu  wote  zaidi ya  watatu  waliokuwemo  wametoka  wakiwa hai ,huku meneja  wa uwanja  wa Ndege Nduli akigoma kuzungumzia  chochote  juu ya ajali  hiyo .

Jitihada za mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  kufika katika  uwanja  huo hazikuweza  kuzaa matunda ya kupata  ukweli wa akina nani walikuwemo katika  ndege hiyo na chanzo  cha ajali ni nini

MwanaHalisi Litafunguliwa Lini?


Magazeti Leo Jumatano Vichwa Vikubwa Leo Jerry Muro Kortini Tena,Vigogo Tazara Wapewa Dhamana Na Tanesco Watengeneza Mgao Kwa Hujuma.












UGANDA YATANGULIA ROBO FAINALI CECAFA TUSKER CHALLENGE


Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen (kulia) akishuhudia kwa makini mchezo wa Kundi A, kati ya Uganda na Ethiopia, Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Kagame Uwanja wa Mandela, Namboole, Kampala, Uganda. Wengine kushoto kwake ni Michael Mukunza wa Executive Solutions, Waratibu wa udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager kwa Stars na Kocha Msaidizi, Sylvester Marsh. 

Hatari kwenywe lango la Ethiopia

Kipa namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira akiwa jukwaani kufuatilia mchezo huo, kushoto ni kimwana aliyekuwa naye. Abbel hatacheza tena mashindano haya baada ya kuumia kwenye mechi ya ufunguzi na Kenya jicho lililovimba kulia.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Mdenmark Kim Polusen (kulia) akijadiliana na Msaidizi wake, Sylvester Marsh wakati mchezo huo.

Angalia PICHA 5...za GARI ALILO PATA NALO AJALI MAREHEMU SHARO MILIONEA









Msanii Wa Bongo Movie John Maganga Azikwa




 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM,  Nape Nnauye akitoa salam za Chama, kwenye msiba wa msanii, Joseph Maganga, Mwananyamala, Dar es salaam. Maganga alifariki Jumamosi hii
 Nape (kulia) akiwa kwenye msiba huo
  Msanii wa Bongo Movie,  Husna Maulidi 'Lishez', akitulizwa na wenzake, Babby Candy na  Ketty wakati akilia kwa uchungu, wakati wa kuaga mwili wa Msanii wa Bongo Movie, marehemu  John Maganga
  Wasanii wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John Maganga, wakati wa kuaga mwili huo, Mwananyamala, Dar es Salaam
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Stephen Maganga, baba wa msanii John Maganga wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyama, Dar es salaam
Nape akizungumza na Rais wa Chama Cha Bongo Movie wakati wa msiba huo

Wafanyabiashara wa Dar Watiwa Mbaroni Zanzibar Wakiwa na Madawa ya Kulevya Kibao.



 

Mzigo wa dawa za kulevya.Picha na Maktaba.

Wafanyabiashara wawili wa Jijini Dar es Salaam, wametiwa mbaroni Visiwani Zanzibar baada ya kupatikana wakiingiza madawa ya kulevya kwa njia ya majini.
Naibu Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Othuman Chande Othmani (22) mkazi wa Kinondoni na Abubakari Muharami Bakari(33) mkazi wa Temeke.
Kamanda Ilembo amesema kuwa watuhumiwa hao wote wamekamatwa katika Bandari ya Zanzibar walipokuwa wakiwasili kwa boti kutoka Dar es Salaam wakiwa na madawa hayo ya kulevya aina ya Heroine.
Amesema kuwa Mtuhumiwa Abubakari alikamatwa juzi saa 3.00 asubuhi akiwa na kifurushi kimoja likichokuwa na madawa hayo ambapo mwenzake Othman yeye ametiwa nguvuni leo saa 3.00 asubuhi akiwa na vifurushi viwili vya madawa hayo aina ya Heroine.
Kamanda Ilembo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa  hao kunatokana na kuimarishwa kwa ulinzi na upekuzi wa hali ya juu uliopo katika maeneo ya viwanja vya ndege na bandari ya Zanzibar.
Amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zao za kupatikana na madawa ya kulevywa visiwani hapa.
Amewataka wananchi wakiwemo wasafiri wa ndege na boti wanaoingia na kutoka katika visiwa vya Unguja na Pemba kuacha kulalama na kuona kuwa wanapopekuliwa wanabughudhiwa.
Ammesema maeneo yote ya Viwanja vya Ndege na Bandarini Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimeimarisha ulinzi ili kuhakikisha kuwa hakuna kitu cha hatari kinachoingizwa Visiwani humo.
Mbali ya Madawa ya kulevya na silaha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepiga mariufuku uingizwaji wa mifuko ya plastiki ya aina zote na kwamba kwa yeyote atakayepatikana na mfuko wa plastiki atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Kwa siku za hivi karibuni baadhi ya wasafiri wamekuwa wakilalamikia hali ya upekuzi unaoendeshwa katika maeneo ya Viwanja vya Ndege na Bandari na hali wanayoona kuwa ni usumbufu kwao.

Fastjet yaja na Nauli Nafuu katika Usafiri wa Anga.



 

Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Bw. Ed Winter  akizungumza kabla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya usafiri wa Anga wa bei nafuu kutoka shirika la ndege la Fastjet Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuanzia Alhamis ya Tarehe 29 mwezi huu Safari za Fastjet zitakuwa mara mbili kwa kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza zote zikiwa safari zenye wasafiri wengi wa ndani.
Aliongeza Nauli zitakuwa za wastani wa dolla USD 80, lakini zinaanzia bei ya chini kabisa Dolla USD 20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali kwa wateja watakowahi kununua tiketi.
 Winter alisema “Leo ni siku ya kusisimua sana, na siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika, shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama na ubora.”
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Fastjet nchini leo ambapo alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kupanua wigo wake wa ushirikiano na taasisi za watu binafsi katika sekta ya Anga nchini.
 Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya nchi na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bw. Fadhili Manongi.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Tizeba  (wa pili kushoto) akiwaongoza wageni waalikwa kuelekea sehemu maalum ya uzinduzi.
 Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakielekea kupanda  ndege aina ya Airbus A319.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba na Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Bw. Ed Winter wakipanda ndege kuashiria uzinduzi rasmi wa safari za ndege hiyo nchini Tanzania.
 Wahudumu nadhifu wa ndege mpya ya Fastjet wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Fatsjet Afrika Bw. Kyle Haywood (katikati).
Welcome on Board Ladies and Gentlemen.
Wageni waalikwa wakikwea pipa kuanza safari.
Cabin Crew wa Fastjest Bi. Victoria Maleko akitoa huduma ya vinywaji kwa wageni waalikwa.
Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”
Fastjet itakuwa ikiendeshwa na timu yenye uzoefu wa safari za ikiongozwa na Ed Winter, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa zamani wa kampuni ya easyjet na mkurugenzi mwanzilishi wa shirika la ndege ya bei nafuu la Go, Afisa Biashara Mkuu Richard Bodin, Mkurugenzi wa zamani wa Mikataba wa easyJet na Mkurugenzi wa Biashara wa shirika la ndege la bei nafuu la Jet2.com, Mkurugenzi wa Uendeshaji Rob Bishton, Rubani Kiongozi & Mkuu wa Shughuli za Ndege wa easyJet na Meneja Mkuu wa Afrika Kyle Haywood, amabye aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Air Uganda.
Shirika hili la ndege linaendeshwa chini ya leseni ya chapa ya easyGroup Holdings Limited na Sir Stelios Haji-Ioannou, mwanzilishi wa shirika la ndege kinara kwa nauli nafuu, EasyJet.