Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Bw. Ed Winter  akizungumza kabla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya usafiri wa Anga wa bei nafuu kutoka shirika la ndege la Fastjet Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Alisema kuanzia Alhamis ya Tarehe 29 mwezi huu Safari za Fastjet zitakuwa mara mbili kwa kutwa kwenye ruti zake mbili za mwanzo Dar es Salaam-Kilimanjaro na Dar es Salaam-Mwanza zote zikiwa safari zenye wasafiri wengi wa ndani.
Aliongeza Nauli zitakuwa za wastani wa dolla USD 80, lakini zinaanzia bei ya chini kabisa Dolla USD 20 kwa safari ya kwenda, kabla ya kodi za serikali kwa wateja watakowahi kununua tiketi.
 Winter alisema “Leo ni siku ya kusisimua sana, na siyo tu kwa fastjet, bali kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla. Kwa miaka mingi tasnia ya safari za anga Afrika imekosa huduma bora, na kulegalega nyuma ya kwingine duniani. Ustawi wa mapato umeongeza fursa za watu kuwa na mapato ya ziada, na pamoja na kwamba hilo limeambatana na mahitaji makubwaya usafiri wa anga, bado watu baraniAfrika wamekosa fursa za usafiri wa anga wanaoumudu na kuuamini. fastjet sasa itaziba pengo hilo na kwakuwaletea Watanzania, na hasa bara zima la Afrika, shirika la kwanza la ndege la nauli nafuu, likiwa na safari za kituo hadi kituo, na lenye kujiendesha kwa viwango vya kimataifa vya usalama na ubora.”
Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba (Mb) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi rasmi wa Fastjet nchini leo ambapo alisisitiza kwamba Serikali itaendelea kupanua wigo wake wa ushirikiano na taasisi za watu binafsi katika sekta ya Anga nchini.
 Pichani Juu na Chini ni baadhi ya waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya nchi na wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.
 Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Bw. Fadhili Manongi.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Tizeba  (wa pili kushoto) akiwaongoza wageni waalikwa kuelekea sehemu maalum ya uzinduzi.
 Baadhi ya wageni waalikwa na waandishi wa habari wakielekea kupanda  ndege aina ya Airbus A319.
 Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Dkt. Charles Tizeba na Afisa Mtendaji Mkuu wa fastjet Bw. Ed Winter wakipanda ndege kuashiria uzinduzi rasmi wa safari za ndege hiyo nchini Tanzania.
 Wahudumu nadhifu wa ndege mpya ya Fastjet wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mkuu wa Fatsjet Afrika Bw. Kyle Haywood (katikati).
Welcome on Board Ladies and Gentlemen.
Wageni waalikwa wakikwea pipa kuanza safari.
Cabin Crew wa Fastjest Bi. Victoria Maleko akitoa huduma ya vinywaji kwa wageni waalikwa.
Uamuzi wa fastjet kujikita kwenye ndege aina ya A319 pekee ni kidhihirisha ufanisi, kuaminika na kustahili kwa ndege za aina hiyo kwa ajili ya safari za nauli nafuu barani Afrika na haswa kusini mwa Jangwa la Sahara. Ndege hiyo itakayotumiwa na fastjet inaoongoza kwenye mauzo ya ndege aina ya Airbusna inayo safu mbili za viti,, fastjet imezingatia kuleta viwango vipya vya starehe na unafuu wa gharamakwenye soko la Afrika ambalo linatarjiwa kuongezeka mara dufu karikakipindi cha miaka 20 ijayo .”
Fastjet itakuwa ikiendeshwa na timu yenye uzoefu wa safari za ikiongozwa na Ed Winter, Afisa Mwendeshaji Mkuu wa zamani wa kampuni ya easyjet na mkurugenzi mwanzilishi wa shirika la ndege ya bei nafuu la Go, Afisa Biashara Mkuu Richard Bodin, Mkurugenzi wa zamani wa Mikataba wa easyJet na Mkurugenzi wa Biashara wa shirika la ndege la bei nafuu la Jet2.com, Mkurugenzi wa Uendeshaji Rob Bishton, Rubani Kiongozi & Mkuu wa Shughuli za Ndege wa easyJet na Meneja Mkuu wa Afrika Kyle Haywood, amabye aliwahi kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Air Uganda.
Shirika hili la ndege linaendeshwa chini ya leseni ya chapa ya easyGroup Holdings Limited na Sir Stelios Haji-Ioannou, mwanzilishi wa shirika la ndege kinara kwa nauli nafuu, EasyJet.