Kikosi cha Simba leo |
Kikosi cha Azam leo |
Kipre Balou wa Azam kulia akiwania mpira wa juu na Abdallah Seseme wa Simba |
Samir Hajji Nuhu wa Azam akiwatoka wachezaji wa Simba |
Miraj Adam wa Simba akiuwahi mpira dhidi ya Hajji Nuhu wa Azam |
Humphrey Mieno wa Azam aliyeenda hewani kuifungia bao la kwanza timu yake |
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Humphrey Mieno kufunga bao la kwanza |
Paul Ngalema wa Simba akimdhibiti Uhuru Suleiman wa Azam FC |
Ibrahim Mwaipopo anatoa pasi huku akiwa amebanwa na wachezaji wa Simba SC |
Kipa wa Simba SC, William Mweta akiwa amedaka mbele ya mshambuliaji wa Azam, Brian Umony huku beki wake Paul Ngalema akiwa tayari kutoa msaada kulia |
Seif Abdallah wa Azam akiwatoka mabeki wa Simba |
Ramadhani Mkipalamoto akiwatoka mabeki wa Azam |
Kipre Balou akimiliki mpira mbele ya Jonas Mkude wa Simba |
Haruna Chanongo akitoa pasi kwa kichwa mbele ya Ibrahim Mwaipopo |
Miraj Madenge wa Simba, akimiliki mpira mbele ya Himid Mao wa Azam |
Himid ameosha mbele ya Madenge |
Madenge akimpongeza Rashid Ismail kufunga bao la kwanza la Simba SC |
Mwadini Ally amedaka mbele ya beki wake Himi Mao, huku Ramadhani Mkipalamoto akifukuzia |
David Mwantika wa Azam akimdhibiti Mkipalamoto wa Simba SC |
Samih Hajji Nuhu amempitia Mkipalamoto na mpira wake |
Daktari wa Simba SC akimtoa nje beki Hassan Hatibu baada ya kuumia kiasi cha kushindwa kuendelea na mchezo |
Mkipalamoto amemlamba chenga Himid Mao, anaondoka... |
Lakini shuti lake lilidakwa na Mwadini...lilikuwa bao la wazi sana alikosa |
Gaudence Mwaikimba akipiga mpira kichwa ambao ulitoka nje sentimita chache |
Hatari langoni mwa Simba SC |
Lakini salama... |
Himid Mao akiwa ametoa mpira nje kupunguza kasi ya Haruna Chanongo wa Simba SC |
Mwantika amezuia, anaanza kugeuka taratibu |
Miraj Madenge akishangilia baada ya kuifungia Simba bao la pili |
Kutoka kulia ni Hassan Khatibu na Rashid Ismail wakicheza na Miraj Madenge kumpongeza kwa kufunga bao la pili |
Mkipalamoto akitafuta mbinu za kumtoka Mwantika |
Hapa ni wakati Azam ikiwa nyuma kwa 2-1, tazama sura ya kocha wa Azam, Muingereza Stewart Hall ilivyokuwa |
Brian Umony akiwa benchi baada ya kutolewa |
Kipa wa Simba SC, William Mweta akigagaa mpira ukiwa nyavuni...ni baada ya mkwaju wa penalti wa Joackins Atudo kuipatia Azam bao la kusawazisha |
Wachezaji wa Azam Seif Abdallah kulia na Humphrey Mieno kushoto wakiwa kwenye benchi baada ya kutolewa |
Makocha wanne wa kigeni wa Azam wakiwapa mawaidha wachezaji wao kabla ya kuingia kumalizia dakika 30 za nyongeza |
Kuna wakati ilibidi Stewart Hall aombe ushauri kwa mchezaji wake wa akiba, Luckson Kakolaki kushoto ambaye anamuambia cha kufanya, bila shaka ilikuwa ushauri mzuri na ndiyo maana timu ilishinda |
Shujaa wa Azam, Malikqa Ndeule akiwa amebebwa juu juu | SOURCE http://bongostaz.blogspot.com/ |
No comments:
Post a Comment