Ndugu na jamaa wakiwa na majonzi msibani kwa marehemu Omar Omar, Temeke-Mikoroshini jijini Dar.
Marehemu Omar Omar enzi za uhai wake.
Dada wa marehemu (hakufahamika jina lake mara moja) akiwasiliana na ndugu wengine ambao hawapo msibani.
Mwanamuziki
wa kizazi kipya, Dully Sykes, mwenye T-shirt ya mistari (nyuma
katikati) akibadilishana mawazo na wazee msibani hapo.
Meneja wa marehemu, Bonga Ticha (kushoto) akiwa na meneja wa kundi la muziki la Wanaume Family, Mkubwa Fella.
Baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya na mameneja wao wakiwa msibani hapo.
----------------------
WAOMBOLEZAJI
mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, leo
wamekusanyika nyumbani kwa mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya mnanda,
Omar Omar Mfungilo, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao
Temeke-Mikoroshini, Dar es Salaam. Kwa mujibu wa baba mdogo wa
marehemu, mzee Yusufu Ally Mfungilo, marehemu Omar anatarajiwa kuzikwa
kesho saa saba mchana huko Temeke.
No comments:
Post a Comment