Baada ya kupata nafuu
anakuja kumalizia hasira zake kwa wanafunzi kwa kumkamata mmoja na kumpa kipigo
cha nguvu hadi askari wenzake walivyopiga kelele ndipo alimwachilia mwanafunzi
huyo
|
Hakuishia
hapo aliwafuata pale walipoamrishwa kukaa akawa anamchomoa anaemtaka na
kumpa kipigovile alivyojiskia ili amalizie hasira zake. |
|
Kumbuka kipigo hicho kinafanyika mbele ya kituo cha polisi huku kukiwa na ulinzi mkali umeimarishwa. |
|
Alichagua kama maembe au mpira na kuchezea alivyotaka! |
BAADA
ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda
wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao
hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa,
waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka
mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi
wengi wao walielekea huko.
Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa
maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo
ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa
na kuumia wengine walipoteza fahamu.
Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa
na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya
utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova
aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya
tarehe 30 mwezi huu.
|
Askari
Polisi ambaye hakuwa kwenye sale za jeshi hilo akimsulubu mmoja wa
wanafunzi wa IFM baada ya kudhibitiwa kwenye eneo la kituo cha Polisi
Kigamboni walipofika kutaka kulazimisha kufanyika mkutano wao na kamanda
Kova badala ya eneo lililopangwa kwenye viwanja vya Machava. Wanafunzi
hao walikamatwa baada ya kupigwa mabomu ya machozi kwenye eneo hilo na
kukamatwa kama kuku wa mdondo. |
|
Askari
wa kike na wakiume wakimdhibiti kwa bakora na marungu mwanafunzi wa
chuo cha IFM (mwenye nguo za blue) baada ya kumchomoa kwenye jengo
alilojificha ili kukwepa mabomu ya machozi. |
|
Kundi
la wanafunzi walishikwa kama kuku wa mdondo baada ya kupigwa mabomu ya
machozi na kujikuta wakijificha sehemu moja kundi zima hali iliyosabisha
kutembezwa kichurachura hadi kwenye kituo cha Polisi cha Kigamboni. |
|
Mwanafunzi
huyu alilala kabisa na kupoteza fahamu baada ya kuzidiwa na moshi wa
mabomu ya machozi yaliyopigwa kwenye eneo la kituo hicho cha Polisi. |
|
Mwanafunzi
huyu alidondoka kwenye Difenda baada ya Defenda hilo kujazana wanafunzi
wengi ambao wakipelekwa kwenye kituo cha Polisi Kigamboni. |
|
Baada
ya kitikisa mabomu yakutosha kwenye baa pembeni ambako walijificha
wanafunzi hao walitaka amani itawale huku wakikimbilia gari la polisi
ili wajisalimishe. |
|
Huyu
alishikiliwa mapema mara baada ya mabomu kuanza kupigwa, huku akionja
joto ya jiwe ya askari hao ambao walionekana kuwa na uchu wakupiga. |
|
Hapa
amri ilikuwa ni mwendo wa kutembea kwa magoti lakini kipigo cha bakora
kililazimisha wengine kuwaruka wenzao ama kuwakanyaga wale waliochini. |
|
Huyu hakujiweza kabisa mabomu yalimchanganya na kudondoka toka kwenye Difenda ya Polisi.
|
Virungu vilitumika kushindilia watu kwenye Difenda. |
|
Hiki
ndicho kikosi Kamili kilichotumia dakika 15 kusambaratisha kundi la
wanafunzi zaidi ya 800 walioweka kambi ya muda mfupi kwenye kituo cha
Polisi Kigamboni . Picha zote na Saidi P |
|
|
No comments:
Post a Comment