Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, January 21, 2013

UKWELI WA AFYA YA DCI MANUMBA KUJULIKANA LEO.



DCI ROBERT MANUMBA.

UKWELI kuhusu hali ya Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, utajulikana leo wakati akiendelea kuwa chini ya uangalizi maalumu wa wauguzi na madaktari wa Hospitali ya Aga Khan.

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso, aliyekuwapo hospitalini hapo, alisema hadi sasa wanasubiri kauli ya daktari wake na kisha watajua la kufanya.

Alisema hivi sasa hawawezi kuchukua uamuzi wa aina yoyote hadi pale madaktari watakapotoa mapendekezo yao ya kitaalamu.

“Bado anaendelea na matibabu na yupo chini ya ungalizi maalumu lakini kwa sasa tunasubiri uamuzi wa madaktari wake wanaomtibia ambao watatoa tamko lao kesho (leo), hivyo ninaomba tuvute subira katika kipindi hiki

No comments:

Post a Comment