Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, February 3, 2013

MWENYEKITI WA CCM DK JAKAYA KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO MAADHIMISHO YA MIAKA 36 YA CCM MKOANI KIGOMA



22Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Dk. Jakaya Kikwete akizungumza na wana CCM katika makao makuu ya CCM Mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza Matembezi ya mshikamano ya kuadhimisha miaka 36 ya chama hicho yanayofikia kilele leo kwa  sherehe kubwa kwenye uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Chama cha Mapinduzi CCM kinahitimisha sherehe hizo baada ya Sekretarieti yake ikiongozwa na Katibu Mkuu wa chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kufanya shughuli mbalimbali za kukagua miradi inayotekelezwa na Serikali mkoani Humo.
23Wananchi mbalimbali waliojitokeza katika maandamano hayo wakimshangilia Rais Jakaya Kikwete wakati alipokuwa akiongea nao.
9Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akijiandaa pamoja na viongozi wengine wa chama wakijiandaa tayari kwa kuanza matembezi ya mshikamano mjini Kigoma leo asubuhi.
10Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk. Rais Jakaya Kikwete akiongoza  viongozi wengine wa chama katika  matembezi ya mshikamano yaliyofanyika leo mjini Kigoma  asubuhi.
12Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kulia akiwa na Edward katika matembezi hayo.
13Matembezi ya Mshikamano yakielekea ofisi ya CCM mkoani Kigoma.
15Brass Band ya Jeshi la Polisi ikongoza matembezi hayo leo asubuhi.
16Wananchi mbalimbali wakiwa wamejipanga kando ya barabara wakati matembezi hayo yakipita.
17Wananchi mbalimbali wakiwa wamejipanga kando ya barabara wakati matembezi hayo yakipita.
1Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kimataifa akizungumza jambo na Katibu Mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdurahman Kinana kulia ni Katibu wa Halmashauri kuu Oganizesheni Mohamed Seif Khatib.
2Kutoka kulia ni Juma Kengele, Ahmed,  Michuzi, Adam na Othman wakishoo Love kwa picha.
3Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akimsiliza Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM.
4Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro akisalimiana na Dk. Rajab Rutengwe Mkuu wa mkoa wa Katavi.
6Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Siasa na Uhusiano wa Kamataifa Dk. Asha-Rose Migiro akizungumza  Mkuu wa Wilaya ya Kobondo Ndugu Venance Mwamoto, Katikati ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Oganizesheni.
7Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdurahman Kinana akimsikiliza Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Mzee Philip Mangula, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Mwigulu Nchemba.
8Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara kabla ya kuanza kwa maandamano hayo leo asubuhi.
19Wananchi mbalimbali wakiwa wamejitokeza barabarani wakati maandamano hayo yakipita kuelekea Ofisi za  CCM Mkoa wa Kigoma.
24Kutoka Kulia ni Dk. Rajab Rutengwe Kanali Fabian Masawe Mkuu wa mkoa wa Kagera na mdau Alice wakiwa katika picha ya pamoja baada ya maandamano hayo.
source  full shangwe

No comments:

Post a Comment