Wameuawa
kisha kuchinjwa na kuchomwa moto ndivyo miili ya marehemu wanaodhaniwa
kuwa ni majangiri wa wanyama poli inavyoonekana ilipofikishwa
kuhifadhiwa katika hospital ya Mvumi Dodoma.
Mwili
wa Mtu anayedhani wa kuwa ni Jangili ukiwa umehalibika baada ya kuuawa
kuchinjwa na kuchomwa moto katika chumba cha kuhifadhia maiti mvumi
Dodoma.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime akiwaonyesha waandishi wa Habari
meno 73 ya tembo yenye thamani ya zaidi 225 mil ambayo ni sawa na tembo
36 pamoja na Gari aina ya Noah NO T 983 BZJ waliokamata juzi katika
kijiji cha Miganga mvimi wilayani Chamwino Dodoma.
Kamanda
wa polisi Mkoa wa Dodoma David Misime akifafanua jambo mbele ya
waandishi wa Habri kuhusu tukio la vifo vya watu watatu wanaodhaniwa
kuwa ni majangili waliouawa na wananchi katika kiji cha miganga Mvumi
Dodoma pembeni ni Gari aina ya Noah No T 983 BZJ walilokuwa wakilitumia
na kuku meno 73 ya Tembo.
Na John Banda, Dodoma
MAJANGILI
watatu wa nyara za serekali wameuawa kwa mishale yenye sumu na kisha
miili yao kuchomwa moto na wananchi katika purukushani na polisi
walipokuwa wakijaribu kukimbia ili kutorosha meno ya tembo.
Tukio
hilo lilitokea jioni ya alhamis wiki hii katika kijiji cha Miganga kata
ya mvumi wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambapo miili yao ilikutwa
ikiwa imehalibika kutokana na kuchomwa moto.
Akizungumzia
tukio hilo Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema
majangili hayo yaliuawa na wanachi wenye hasira kali kwa zana mbalimbali
za kijadi walipokuwa wanakimbilia polini ili kujiokoa na mkono wa
polisi.
Misime
alisema jeshi hilo lipokea taarifa kutoka kwa wananchi wema kuwa
kulikuwa na Gali likitokea Manda likiwa na Meno ya Tembo na kisha
kuweka mtego katika kijiji cha mwitikila ambapo waliona gali aina ya
NOAH T 983 BZJ na kulisimamisha na Dereva wa Gali hilo alifanya kama
anapunguza mwendo na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.
‘’Polisi
wakishirikiana na wananchi walianza kulifukuza walipofika kijiji cha
Miganga Mvumi polisi walifanikiwa kupiga Risasi tairi moja ya kushoto na
hivyo watu watatu waliokuwemo ndani gari hilo waliruka na kutawanyika,
wananchi waliojichukulia sheria mkononi waliwashambulia kuasi cha
kupoteza maisha yao’’, alisema
Aidha
kamanda Misime alisema baada ya kulipekua Gari hilo walikutaMeno 73 ya
Tembo yenye uzito wa kilo 255.9 yakiwa na thamani ya zaidi ya TSH 225
mil pamoja na hati ya mashitaka [CHARGE SHEET] ambayo ni kesi ya
kuhujumu uchumi namba 4/2012 iliyokuwa imefunguliwa katika mahama yam
panda mkoa wa katavi na Leseni ya Udereva na 4000692535 Aboubakar Peter
huku wakihisi ni mmoja ya waliouawa.
Alisema
walikuwa wameshitakiwa kwa kosa la kupatikana na Meno 3 ya Tembo Tarehe
17.06.2012 na maafisa wanyama poli katika eneo la Msaginya Wilaya ya
Mlele mkoa wa katavi majina ya walikuwa wameshatakiwa ni Joseph Marius
[NGONDO] 59 mkazi wa maili mbili Dodoma, Aboubakar Mhina 25 mkazi wa
Mkuhungu Dodoma, Msafiri Milawa 36 mkazi wa Nkuhungu Dodoma na Petro
Mtipula 55 mkazi wa mpanda.
Kamanda
alitoa wito kwa wananchi wasijichukulie Sheria mikononi kwani kwa
kufanya hivyo ni kupoteza ushahidi na inawawia vigumu polisi kupata
mtandao inayohusika na matukio kama hayo.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJAPURE BLOG
No comments:
Post a Comment