Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
Wanariadha
kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za
Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Wakenya
walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji wao
Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za mwaka
huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna Joseph
alebeba Medali ya Dhahabu.
Nafasi ya
pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor, Onesmo
Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice Muchiri,
Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.
No comments:
Post a Comment