Na Mroki Mroki-Father Kidevu Blog-Moshi
Wanariadha
kutoka Nchini Kenya wameendeleza Umwambawao katika mbio za Nyika za
Kilimanjaro ‘Kilimanjaro Marathon 2013’ zilizofanyika leo mjini Moshi
mkoani Kilimanjaro.
Wakenya
walidhihirisha umwamba katika Mbio za Kilometa 42 baada ya Mkimbiaji
wao Kipsang Kipkemoi kunyakua nafasi ya kwanza katika mbio hizo za
mwaka huu upande wa wanaume na Wanawake ilinyakuliwa na Mwana dada Edna
Joseph alebeba Medali ya Dhahabu.
Nafasi
ya pili hadi ya tano kwa wanaume ni Julius Kilimo, Dominick Kiagor,
Onesmo Maithiya Loshile Moikari ambapo upande wa wanawake ni Eunice
Muchiri, Frida Too, Rosaline David na Jane Kenyara.
Aidha
katika mbio za Kilometa 21, Kenya ilitamba tena kwa upande wa wanaume
baada ya wakimbiaji wake watatu kushika nafasi za juu ambapo Mshindi
alikuwa ni Silah Limo huku nafasi ya pili ikienda kwa Bernard Kiprotich
na nafasi ya tatu ikienda kwa Charles Ogari.
Mtanzania
Dickson Marwa alinyakua nafasi ya nne na nafasi za tano na sita zikenda
Tena Kenya kwa wakimbiaji Peter Kusgei na Evans Taigey nafasi ya saba
ilishikwa na Mtanzania Stephano Huche na kuporwa tena na Kenya nafasi ya
nane iliyoenda kwa Patrick Wambugu aliyekimbia mbele ya watanzania
wawili waliofunga hesabu ya wakimbiaji kumi bora ambapo namba tisa
alikuwa Said Makula na kumi alikuwa Peter Sule.
Shangwe
ya watanzania iliibuliwa na Mwana dada Sara Makera Ramadhan baada ya
kunyakua medali ya dhahabu kwa kuibuka mshindi wa kwanza mbele ya mkenya
Vicomi Chepkemoi huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na mtanzania mwingine
Failuna Makanga.
Nafasi
ya nne ilienda kwa Joyce Kiplimo wa Kenya aliyefuatiwa na mwenzake
Pauline Muchiri kasha Mtanzania Catherine Tuku alishika nafasi ya sita
na zilizosalia hadi nafasi ya kumi zikienda kwa Nchi ya Kenya ambao ni
Nancy Kotch, Jacinta Mboani, Florence Cheruiyot na Phylas Jelagat.
Jumla ya wakimbiaji 65000 walishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon 2013.
Wakimbiaji wa Kenya wakipongezana baada ya kufanya vizuri katika mbio hizo.
Mfukuza
Upepo kutoka Nchini Kenya na Mshindi wa Medali ya Dhahabu katika Mbio
za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo katika Uwanja
wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Eunice
Muchiri akikimbia na kumaliza wapili mbio za Kilimeta 42 Wanawake,
katika Mbio za Kilimanjaro Marathon akienda kumaliza mbio hizo hii leo
katika Uwanja wa Michezo wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi.
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Kim Poulsen akimaliza
kukimbia Kilometa 21 katika mbio za nyika za Kilimanjaro 2013. Poulsen
amedhihirisha kuwa ni mwanamichezo na kuwa kocha wa Kwanza wa Timu ya
Taifa kushiriki mbio hizo tangu kuanzishwa kwake miaka 10 iliyopita.
Wakimbiaji mbalimbali wakishiriki katika mbio hizo leo mkoani Kilimanjaro.
MBIO ZA VODACOM ZANOGESHA MSIMU WA KILIMANJARO MARATHON
Baadhi
ya washiriki wa mbio kujifurahisha za”Vodacom 5KM fun run wakishiriki
katika mbio hizo ambazo ni sehemu yam bio ndefu za Kilimanjaro Marathon
No comments:
Post a Comment