Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 5, 2013

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UKARABATI WA BARABARA YA NYAGUGE-MUSOMA



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, wakati alipotembelea kujionea mashine za kusaga mawe, zilizopo Kijiji cha Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo. Kushoto ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na Mbunge wa Butiama Vijijini, Nimrod Mkono, baada ya kusikiliza maelezo kutoka kwa Eng. Sabyasachi Kar, kuhusu mashine za kusaga mawe wakati alipotembelea kuona mashine hizo, zilizopo Kijiji cha Sabasaba Irimba, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara, iliyo sambamba na Uwekaji jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma,leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Dr. John Ndunguru, wakati alipowasili kuweka jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal na Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya ngoma ya asili, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. Jhn Pombe Magufuli, wakifurahia burudani ya muziki wa dansi kutoka kwa bendi ya Msondo Ngoma, wakati walipowasili eneo la kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akivishwa vazi la Jadi na mzee wa Mkoa wa Mara, Thomas Sura, wakati akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara na kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakifurahia vazi la Jadi baada ya kukabidhiwa na mzee wa Mkoa wa Mara, Thomas Sura, wakati wakiwa katika ziara yao ya siku mbili mkoani Mara na kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
Wasanii wa Kikundi cha sanaa wakitoa burudani wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo Feb 4, 2013. Jiwe hilo limewekwa na Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha Sanaa za asili, wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo Feb 4, 2013. Jiwe hilo limewekwa na Makamua wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal.
 Ilikuwa ni burudani ya kutosha kutoka kwa kikundi hicho.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma leo Feb 4, 2013 wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuweka Jiwe la Msingi ukarabati wa Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa Jiwe la Msingi ukarabati wa  Barabara ya Nyaguge-Musoma, sehemu ya kutoka Mpaka wa Mikoa ya Simiyu na Mara hadi Musoma, leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli na Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Gabriel Tupa, kwakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
.

No comments:

Post a Comment