MwananchiJohannesburg.
Mkurugen-zi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amezung-umzia
ugonjwa wake ambao ulisababisha kutojitambua kwa siku 42 na kwamba sasa
anaendelea vizuri.
Kwa sasa
Manumba ambaye amelazwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu, anaendelea
vizuri na sasa anafanya mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea kama
sehemu ya matibabu yake.
“Kwa sasa
ninashukuru naendelea vizuri, nina-washukuru madaktari wa hapa ambao
wamejitahidi maana ni kama watu wal-ishakata tamaa kwamba siwezi
kupona,” alisema Manumba alipozungumza na Mwananchi katika Hos-pitali ya
Millpark alikolazwa jijini Johannesburg.
Alisema
tatizo kubwa lili-lokuwa likimkabili ni ugon-jwa wa malaria kwani
ali-popimwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikutwa na wadudu wa
ugonjwa huo 500.
“Yaani
huwezi kuamini, nilikuwa na wadudu 500 lakini nilikuwa naendelea na kazi
tu kama kawaida, sasa tiba ya malaria ndiyo ilisababisha kuibuka kwa
magonjwa mengine lukuki ambayo yalisababisha nisiji-tambue kwa siku 42,”
alise-ma Manumba.
Manumba anasema ni kwa mkono wa Mungu amepa-ta nafuu kubwa baada ya juhudi kubwa za madaktari katika kupigania uhai wake.
Alipelekwa Afrika Kusini Januari 23, mwaka huu baa-da ya kupata nafuu kidogo.
Alisema
anawashukuru madaktari wote walio-hangaika usiku na mchana katika
hospitali alizolazwa kuanzia Muhimbili na Aga Khan, jijini Dar es
Salaam, kabla ya kusafirishwa kwa ndege maalumu hadi Johan-nesburg,
Afrika Kusini.
Kadhalika
alilimshukuru Rais Jakaya Kikwete kwam-ba ndiye alisaidia kuhara-kishwa
kwa mchakato wa kuhamishiwa jijini hapa kwa ajili ya matibabu zaidi
ambayo yamemrejeshea uzima ambao tayari ulikuwa kama umepotea. “
No comments:
Post a Comment