Mhariri
Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu na Mhariri Mtenaji wa Free Media,
Ansbert Ngurumo wakiwa na Mhariri Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya New Habari (2006)
na Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri, Absalom Kibanda nchini Afrika
Kusini.
Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Jukwaa la
wahariri
Neville Meena aliyeko Afrika Kusini katika Hospitali ya Mirlpak anakopata
matibabu Kibanda
Wapendwa Wahariri,
Tupo katika
hosiptali ya Milpark, Johannesburg nchini Afrika Kusini kumjulia hali Mwenyekiti
wetu, Absalom Kibanda ambaye kama mnavyofahamu anapatiwa matibabu kutokana na
tukio la kushambuliwa kwake.
Pamoja nami,
pia wapo Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Nipashe, Jesse Kwayu na
Mhariri Mtenaji wa Free Media, Ansbert Ngurumo.
Jana (Ijumaa)
kutwa tulishinda naye hosipitalini na kwa ujumla hali yake inaendelea kuimarika
vizuri. Kama tulivyowaarifu tangu juzi, ameanza mazoezi mepesi ya kusimama na
kutembea na anaweza kukaa kwa muda na kushiriki mazungumzo. Kwa
hakika amechangamka na anatia moyo.
Hata hivyo,
bado mwenyekiti wetu ataendelea kubakia hosipitalini kwa matibabu zaidi kama
wanavyoshauri madaktari wake. Jambo la msingi tuendelee kumwombea
katika sala zetu na wale ambao watapata fursa wafike kumjulia hali na kumtia
moyo.
Kwa muda tutakaokuwa hapa tutaendelea kuwajulisha
maendeleo ya afya yake. Pokeeni pia picha ambazo tumepiga tukiwa pamoja naye
hosipitalini akiwa ameketi kwenye kiti.
Credits: AmaniTanzania
No comments:
Post a Comment