1. Kibanda
leo ameingizwa theater ili kuanza kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura
baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe vilivyokuwa katika sehemu
mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na usoni.
2. Upasuaji
huo unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na
jopo la madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda
pia aliumizwa taya lake la kushoto.
3. Kuhusu
jicho lake la kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema
wangetoa uamuzi kuhusu aina ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya
kubaini hali halisi wakati watakapokuwa wakijenga sura yake ambayo
iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati
akipelekwa theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa
kuchukua saa zaidi ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na
kidonda kilichopo kwenye mguu wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni
matokeo ya unyama aliyofayiwa.
5. Jana
Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao
wako Afrika Kusini kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia
hali. Rais Kikwete alisema Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa
tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba wakikamatwa watafikishwa
mahakamani.
Tutaendelea kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee kumwombea ili apone haraka.
--
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 - 555556
No comments:
Post a Comment