Mwanamuziki
Judith Wambura Mbibo aka Lady JayDee , usiku wa kumkia leo amezindua
video yake mpya aliyomshirikishja Mkongwe Mwezake katika medani ya
muziki wa kazazi kipya , Joseph Haule ‘Prof. J’ Video ya Wimbo unaoitwa
kwa jina la ‘JOTO HASIRA’.
Jaydee
alifanya uzinduzi huo katika mgahawa wake wa Nyumbani Longe uliopo
Namanga wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na mamia
ya wapenzi wa Burudani na muziki wa mwana dada huyo.
Uzinduzi huo ulisindikizwa na bendi ya Lady Jaydee ya Machozi Band na kutoa burudani ambayo ilikonga nyoyo za mashabiki wake.
Mbunifu wa Mavazi Asia Idarous akipozi kwa picha na Mdau Bhoke wakati wa onesho hilo.
Mboni Masimba katikati akiwa katika picha ya pamoja na Juma Pinto na Mdau Fred Maeda
Mamaa Shamimu wa 8020fashionblog akiwajibika kwa kupata taswira za onesho hilo.
Mdau Bhoke akipozi kwa picha
Mdau Jane na mdogo wake nao walijitokeza katika uzinduzi huo wa video ya Joto Hasira.
kutoka kulia ni Monica na kutoka kushoto ni Mboni Masimba na Shamimu Mwasha
Juma Pinto kulia na wadau mbalimbali wakishoo Love kwa picha

Lady JayDee akiimba kwa kushirikiana na waimbaji wa bendi ya Machozi bendi anayoimiliki mwenyewe wakati wa onesho hilo.
Mashabiki wa mwanamuziki huyo wakicheza stejini huku wakiwa wamepanga mstari
Dida Wa Mchops akiongoza mashabiki wa mwanamuziki Lady JayDee wakati wakicheza stejini

No comments:
Post a Comment