Taarifa
za ndani kutoka kwenye chanzo cha kuaminika ni kwamba kikao cha
serikali kupitia wizara ya habari na michezo na shirikisho la soka
nchini kuzungumza juu ya suala la serikali kuondoa usajili wa katiba
mpya ya TFF kimeishia kwa serikali kuliagiza shirikisho hilo kuwataarifu
wanachama juu ya mkutano mkuu ndani ya siku 5 zijazo, na kuandaa mkutano wa kufanya mabadiliko ya katiba katika kipindi cha siku 40 zijazo kutoka leo.
Kwenye
kikao hicho TFF iliwakilishwa na Katibu Mkuu Angetile Osiah,
mwanasheria Alex Mgongolwa, Wallace Karia na Mkurugenzi wa michezo
Sunday Kayuni - taarifa za kutoka ndani ya kikao hicho zinasema kwamba
TFF ilionekana haikufuata taratibu za kufanya marekebisho ya katiba na
hivyo serikali ikafikia maamuzi ya kuwaagiza waandae mkutano mkuu wa
wanachama wote wa TFF ili kukidhi matakwa ya kufanya marekebisho ya
katiba.
Pia
baada ya kufanyika kwa mkutano mkuu, serikali imeagiza uchaguzi mkuu wa
shirikisho hilo ufanyike katika kipindi cha siku 40 baada ya mkutano
mkuu kufanyika.
SOURCE SHAFFIHDAUDA
No comments:
Post a Comment