Hatimaye
sakata la kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri, (TEF), Absalom Kibanda, limepata mwanga na watuhumiwa wa
kadhia hiyo wataanikwa hadharani kesho.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema timu
iliyoundwa kuchunguza kutekwa, kuteswa na kujeruhiwa kwa Kibanda, itatoa
taarifa kamili na idadi ya watu waliowakamata kuhusiana na tukio hilo.
Wakati
Kova akieleza hilo, mitandao ya kijamii jana ilieleza kuhusu taarifa za
kukamatwa kwa mtu aliyejulikana kwa jina la Ludovick Joseph kwa tuhuma
za kuhusika kuteswa kwa Kibanda.
Kova
alipoulizwa kuhusiana na taarifa hizo, aliomba apewe muda ili awasiliane
na mwenyekiti wa timu iliyoundwa kuchunguza tukio hilo.
“Tangu
asubuhi nilikuwa Mabwepande, ndiyo nimerudi ofisini muda sio mrefu,
kuhusu hilo nimelisikia kupitia kwa waandishi wenzako walionipigia simu,
nipe muda nilifuatilie,” alisema.
Baada
ya kupigiwa tena, Kova alisema kwa mujibu wa maelekezo aliyopewa na
timu hiyo, haikuwa muda muafaka kulizungumzia suala hilo jana.
No comments:
Post a Comment