Wanachama wakinyoosha mikono kupinga uongozi uliopo madarakani.
Mwenyekiti wa mkutano huo, Mohammed Wandwi, akiongea na wanachama.
Bi Hindu, mwanachama maarufu wa Simba, naye alitoa lake la moyoni kwenye mkutano huo.
Mwanachama Salum Simba, akiushutumu uongozi wa sasa.
Mwanachama mwingine akimchana ‘live’ Aden Rage kuhusu sakata la Mbuyu Twite na Kelvin Yondani.
Wanachama wakitoka kwa amani baada ya kumaliza mkutano.
Askari wakiangalia suala la usalama.
WANACHAMA
wa klabu ya Simba, leo walifanya kikao cha dharura kwenye Hoteli ya
Star Light Mnazi Mmoja jijini Dar na kuung’oa uongozi wa klabu hiyo
uliopo madarakani chini ya Mwenyekiti wake, Ismail Aden Rage kufuatia
mwenendo mbaya wa timu yao.
Wanachama
hao wamekabidhi uongozi wa klabu hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati
ya Fedha, Rahma Kharus ‘Malkia wa Nyuki’ na kumrudisha kiongozi
aliyejiuzulu hivi karibuni, Zacharia Hans Poppe. Wanachama hao wamesema
wanatarajia kuitisha mkutano mkuu na kuwachagua viongozi wapya baada ya
kumalizika kwa Ligi Kuu inayoendelea ili kuepusha kuivuruga timu.
SOURCE:GLOBALPUBLISHER
No comments:
Post a Comment