Barua
zilizokuwa zimetumwa kwa Rais Barack Obama na Seneta wa Mississippi
Senator Roger Wicker zmebainika kuwa na sumu hatari aina ya ricin.
Idara kuu ya upelelezi ya Marekani FBI imetoa taarifa hiyo na barua zilizotumwa kwa viongozi hao wawili zinahusiana.
Barua
hizo zote zilitumwa kutokea Memphis, Tennessee na mtu mmoja mwenye umri
wa miaka 45 amekamatwa Mississippi kuhusiana na barua hizo.
Pamoja
na barua hizo, polisi mjini Washington wanavichunguza vifurushi vitatu
wanavyovitilia mashaka vilivyogunduliwa katika ofisi za majengo ya
seneti.
No comments:
Post a Comment