Wabunge watano wa
Chadema jana walitimuliwa bungeni na kuamriwa kukaa nje ya Bunge kwa
siku tano kutokana na vurugu zilizotokea jana usiku.Wabunge hao ni
Lissu, Hezekiah Wenje (Nyamagana), Highness Kiwia (Ilemela), Joseph
Mbilinyi (Mbeya Mjini) Godbless Lema (Arusha Mjini) na Mchungaji Peter
Msigwa (Iringa Mjini).
Chanzo za
kufukuzwa kwao ni kuwazuia askari wa Bunge kumtoa nje Lissu ambaye
alikuwa ameamriwa kutoka nje na Naibu Spika, Job Ndugai baada ya
kuingilia hotuba ya
Mbunge wa Iramba Mashariki, Mwigulu Nchemba.
Kutokana na
tafrani hiyo, Nchemba hakuweza kuhitimisha hotuba yake hivyo Ndugai
alilazimika kukatisha mkutano wa Bunge.Hata hivyo wakati akiahirisha
mkutano huo, tayari wabunge hao walikuwa wameshatolewa nje baada ya
askari kuongezwa.
Mapema Mbunge wa
Kigoma Mjini (CCM), Peter Serukamba alitoa tusi zito la nguoni wakati wa
hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma, licha ya Spika wa Bunge, Anne Makinda
kupiga mkwara wa kuwashughulikia wabunge watakaorusha matusi.
Mbali na tukio
hilo Lema naye alichafua hali ya hewa baada ya kuwatuhumu viongozi wa
CCM akiwamo Rais Jakaya Kikwete kwa udini, madai ambayo Bunge limempa
siku saba kuyathibitisha.
Lema aliituhumu CCM na Serikali yake chini
ya Rais Kikwete kwa kushindwa kutatua mgogoro wa kidini na badala yake
kuwa kama analikwepa tatizo. Alionya kuwa Taifa linapasuka kwa migogoro
kutokana na viongozi wa Serikali kushindwa kulishughulikia.
No comments:
Post a Comment