Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda (kulia)
akiwa na mshtakiwa mwenzake Saleh Mkadamu wakielekea kupanda basi la
magereza baada ya hukumu ya kesi yao ya uchochezi kuahirishwa hadi Mei
9. Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49 wanakabiriwa na makosa matano
ya kula njama na kuingia kwa jinai katika uwanja namba 311/3/4 kitalu T
uliopo Markaz Chang'ombe na wizi wa vifaa mbalimbali vya ujenzi vyenye
thamani ya Shs milioni 59 mali ya kampuni ya Agritanza.
Saleh Mkadamu akipanda basi kuelekea mahabusu
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akipanda basi la magereza.
Ulinzi mkali kila kona ya mahakama
Msafara
wa magari ya Polisi wakisindikiza gari la magereza lililomchukua Katibu
wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda
wakati wakielekea mahabusu baada ya hukumu ya kesi yao kuahirishwa leo
hadi Mei 9.
Wafuasi
wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa
Ponda wakiwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini
Dar es Salaam leo wakati hukumu ya kesi yake ilipoahirishwa leo.Picha
na Habari Mseto Blog
No comments:
Post a Comment